Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mchungaji kortini akikabiliwa na mashtaka matano Dar

Mshtakiwa Daniel Mgonja akienda kwenye chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Picha na Pamela Chilongola

Muktasari:

  • Raia wa Congo ambaye ni mchungaji, Daniel Mgonja baada ya kusomewa mashtaka matano yanayomkabili alipoulizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Anna Magutu alikiri kutenda makosa hayo.

Dar es Salaam. Raia wa Congo ambaye ni mchungaji, Daniel Mgonja (23) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam akikabiliwa na mashtaka matano likiwemo la kujishughulisha na shughuli za kichungaji bila ya kuwa na kibali.

Wakili wa Serikali, Rafael Mpuya akisoma hati ya mashtaka leo Jumanne, Julai 9,2024 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Anna Magutu amesema Juni 24, 2023 katika ofisi za uhamiaji zilizopo Kurasini jijini humo mshtakiwa huyo aliishi bila ya kuwa na kibali kinachomruhusu kuwepo nchini.

Katika shtaka la pili tarehe na maeneo hayo mshtakiwa huyo alitoa taarifa za uongo ili ajipatoe Kitambulisho cha Taifa (Nida) wakati akijua siyo kweli.

Katika shtaka jingine, tarehe hiyo na maeneo hayo mshtakiwa huyo alitoa nyaraka za uongo ikiwemo cheti cha kuzaliwa na Nida ambavyo alivipata kwa njia ya uongo ili aweze kujipatia hati ya kusafiria.

Mpuya amedai katika shtaka la nne mshtakiwa huyo anakabiliwa na kosa la kuwadanganya maofisa wa uhamiaji wakiwa kwenye majukumu yao ya kazi aliwasilisha nyaraka za uongo na kujipatia hati ya muda ya kusafiria.

Katika shtaka la mwisho mshtakiwa huyo anakabiliwa na kosa la kujishughulisha na shughuli za kichungaji bila ya kuwa na kibali cha kuishi nchini.

Wakili Mpuya baada ya kumsomea mshtakiwa huyo mashtaka yanayomkabili ndipo hakimu Magutu alimuuliza kama mshtakiwa huyo ametenda makosa hayo na amekiri kutenda.

Kesi hiyo inarudi Julai 12, 2024 kwa ajili ya kusomewa hoja za awali.