Melisa John aibuka mshindi wa Airtel Trace Music
Muktasari:
Baada ya kuimba kwa umahiri mkubwa wimbo wa mwanamuziki Mica Paris ujulikanao kama “My One Temptation” Melisa aliweza kuwaaminisha majaji kwamba hakika yeye anastahili kuwa mshindi wa Airtel Trace Music Stars msimu wa 2
Mashindano ya Airtel Trace Music Stars ya taifa yamefikia mwisho ambapo Melisa John alitangazwa kuwa mshindi wakati wa fainalii za shindano hilo lililowashirikisha washiriki watano bora na kufanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Saalam
Baada ya kuimba kwa umahiri mkubwa wimbo wa mwanamuziki Mica Paris ujulikanao kama “My One Temptation” Melisa aliweza kuwaaminisha majaji kwamba hakika yeye anastahili kuwa mshindi wa Airtel Trace Music Stars msimu wa 2
Melisa amejishindia shilingi milion 50 huku mshindi wa pili Nandi Charles akijishindia shilingi milioni 5 na mshindi wa tatu Salim Mlindila akiondoka na shilingi milioni 2
Kufatia ushindi huo Melisa sasa amepata tiketi ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Airtel Trace Music Stars Afrika yatakayoshirikisha washiriki kutoka nchi 9 zikiwemo Niger, DR Congo, Gabon, Kenya, Madagascar, Malawi, Nigeria, Ghana and Zambia yanayotegemea kufanyaka tarehe 11 Juni 2016 , Lagos nchini Nigeria.
Mshindi wa Airtel Trace Music Afrika atapata nafasi ya kupata mafunzo ya muziki na kurekodi video na mwanamuziki nguli na mtunzi wa nyimbo Keri Hilson , Atlanta nchini Marekani
“Nimefurahi sana kuibuka mshindi leo, pamoja na ushindi huu mashindano yalikuwa ni ya ushindani kwani kila mshiriki alikuwa na uwezo wa kuimba na mzuri kwa namna tofauti. Nashukuru Mungu kwa kunifikisha hapa na nawashukuru Airtel kwa kutuandalia jukwaa hili ambapo leo limenifanya niweze kuishi ndoto zangu. Napenda sana kuimba na napenda sana mziki naamini huu ni mwanzo mzuri wa safari yangu ya kuwa mwanamuziki nyota” alisema Mshindi wa Airtel Trace Music Stars 2016 Melisa John
Kwa upande wake Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde alisema “ Airtel inajivunia kuwa sehemu ya kuinua maisha ya vijana wengi, tunaamini kupitia program zetu za kuwawezesha vijana tutagusa maisha ya vijana wengi na kuwawezesha kuzifikia ndoto zao. Tumefurahia mashindano ya mwaka huu yamekuwa na mvuto zaidi na tunampongeza Melisa kwakuibuka kuwa mshindi. Tunamtakia afanye vyema katika michuano ya Afrika nchini Nigeria.”
Katika fainali hizo Mshindi wa Airtel Trace Music Stars Afrika, Nalimi Mayunga alitoa burdani ya nyimbo yake ya “ Nice Couple”na kuweza kuzindua kibao chake na video yake ijulikanayo kama “ Please don’t go away” e inayomshirikisha mwanamuziki nguli kutoka marekani, Akon