Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Meya Moshi aamuru kuvunjwa ukuta ofisi za basi la Kilimanjaro Express

Muktasari:

  • Meya wa Manispaa ya Moshi, Juma Raibu ameagiza kuvunjwa kwa uzio unaozunguka jengo la ofisi za kampuni ya usafirishaji ya mabasi ya Kilimanjaro Express uliojengwa kinyume na sheria za mipango miji.

Moshi. Meya wa Manispaa ya Moshi, Juma Raibu ameagiza kuvunjwa kwa uzio unaozunguka jengo la ofisi za kampuni ya usafirishaji ya mabasi ya Kilimanjaro Express uliojengwa kinyume na sheria za mipango miji.

Raibu ametoa agizo hilo leo, Machi Mosi, mwaka huu baada ya kufika kwenye ofisi hizo baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wakazi wa manispaa hiyo.

Eneo hilo la wazi ambalo limezungushiwa uzio limekuwa likilalamikiwa na wakazi wa Manispaa ya Moshi na wakati mwingine kuleta usumbufu kwa watumiaji wengine barabara.

"Nimemwelekeza Mhandisi wa Tarura Manispaa ya Moshi eneo hili livunjwe mara moja ili wananchi waendelee kukaa hapa kama kawaida bila kubughudhiwa,"amesema Raibu.

Aidha, amesema eneo hilo la wazi limekuwa likilalamikiwa na wafanyabiashara wadogo baada ya kuwekewa uzio na kulifanya kama la kwake.

"Eneo hili ni eneo la umma ambalo lipo chini ya Tarura na mfanyabiashara huyu ameweka uzio eneo lote amelifanya kama la kwake kinyume na sheria kuna taratibu zinazotumika maeneo ya wazi,


"Huu uzio unatakiwa kuondolewa na nimeshaagiza,hili jambo ni fedheha kwa wananchi wangu wa Moshi ,"amesema Raibu.


Wakizungumzia uzio huo, wananchi wa manispaa hiyo wakiwemo madereva taxi wamesema uzio huo kuwekwa kwenye eneo hilo ambalo ni la wazi na lipo karibu na mzunguko wa mnara wa(keep left) ni hatarishi kwa watembea kwa miguu na kwamba linawazuia kufanya biashara zao.