Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Meya Moshi awakabidhi wazabuni wanane kwa Takukuru

Meya Moshi awakabidhi wazabuni wanane kwa Takukuru

Muktasari:

  • Viongozi wa Vicoba nao wamejikuta wakiangukia mikononi mwa Taasisi ya kupambana na rushwa kwa kushindwa kurejesha fedha walizokopa.

Moshi. Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi, Juma Raibu ameagiza kukamtwa kwa wazabuni wanane wanaodaiwa kula fedha za Halmashauri zaidi ya Sh47 milioni pamoja na viongozi wa vikundi 45 vya asasi za kuweka na kukopa (Vicoba).

Viongozi hao wanadaiwa kuwa wameshindwa kurejesha zaidi ya Sh94 milioni walizokopa  tangu mwaka 2015.

Raibu ametoa agizo hilo leo, Machi 31,2021 alipowaita viongozi hao ofisini kwake kutaka kujua hatma ya fedha hizo ambazo walikopewa na Halmashauri ya Manispaa ya Moshi.

"Wote hapa niliowaita mmehujumu fedha za serikali, hili jambo linakera sana haiwezekani tangu mwaka 2015 mpaka leo hamjarejesha fedha hizi mnazodaiwa na Halmashauri zaidi ya Sh94 milioni, hili halikubaliki nawakabidhi leo mikononi mwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mtuambie mnarejeshaje fedha hizi," amesema na kuongeza:

"Naomba muondoke na hawa watu watuambie tunapataje fedha zetu ambazo tuliwapa kwa upendo mkubwa, mimi sina mzaha kwenye fedha za serikali," amesema Raibu.

"Takukuru naomba pia niwakabidhi wazabuni wanane waliokwapua fedha zetu  za  Halmashauri zaidi ya Sh47 milioni watuambie  wanazirejesha hizi fedha za serikali,” amesema Raibu.