Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mkemia adai unga uliokutwa kwa Mushi ni mchanganyiko wa dawa za kutibu magonjwa ya afya akili

Mshtakiwa Dominic Mushi anayekabiliwa na shtaka la mauaji ya mke wake, Diana Hugo akiwa chini ya ulinzi wa askari Magereza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakati kesi yake ilipoitwa kwa ajili ya usikilizwaji. Picha na Hadija Jumanne

Muktasari:

  • Dominic ambaye alikuwa ni Ofisa Mtendaji wa Kata Gongo la Mboto, anadaiwa kumuua mkewe aitwaye  Diana Hugo kwa kumnyonga hadi kufa, tukio analodaiwa kulitenda Oktoba 14, 2024 saa tisa usiku, eneo la Kinyerezi Kichangani, Wilaya ya Ilala.

Dar es Salaam. Mkemia wa Serikali daraja la kwanza, Lowasa Erika, ameiambia Mahakama kuwa uchunguzi alioufanya kwenye mabaki ya unga ulioganda katika bilauli ya plastiki iliyokutwa chumbani kwa mtuhumiwa Dominic Mushi, ulibaini kuwa ni mchanganyiko wa dawa za hospitali, ambazo zikitumiwa kwa wingi zinaweza kusababisha kifo.

Mushi anakabiliwa na shtaka moja la mauaji ya mkewe Diana, tukio analodaiwa kulitenda Oktoba 14, 2024 eneo la Kinyerezi Kichangani, lililopo wilaya ya Ilala.

Diana ambaye alikuwa mfanyakazi wa Benki ya NMB Tawi la Airport, anadaiwa kuuawa na mumewe na mwili wake ulikutwa kitandani ukitoka damu eneo la puani, masikioni na mdomoni.

‎Mshtakiwa huyo anadaiwa katika maelezo yake ya onyo aliyoyatoa Kituo cha Polisi Stakishari, alidai kuwa kelele za kuomba msaada alizokuwa akizitoa mke wake siku hiyo usiku ilikuwa ni mke wake alikuwa anaota.

Lowasa, ambaye ni shahidi wa 11 wa upande wa Jamhuri katika kesi ya mauaji, alidai kuwa mchanganyiko huo ulihusisha dawa mbili: Chlorpromazine, inayotumika kutibu magonjwa ya afya ya akili, na Metronidazole (Flagyl), inayotumika kutibu maambukizi.

Shahidi huyo kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) alitoa ushahidi wake Aprili 22, 2026, katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam iliyoketi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, katika kesi ya mauaji inayomkabili aliyekuwa Ofisa Mtendaji wa Kata ya Gongolamboto, Dominic Mushi.

Lowasa ametoa ushahidi huo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Hassan Makube aliyepewa Mamlaka ya nyongeza kusikiliza kesi hiyo ya mauji.

Akiongozwa kutoa ushahidi wake na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Brenda Massawe akishirikiana na wakili wa Serikali Hakme Pembeni, shahidi alidai Oktoba 22, 2024 akiwa katika ofisi za (GCLA) jijini Dar es Salaam, alipokea kielelezo kutoka ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Kipolisi wilaya ya Ukonga, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Ally Kweka.

“Kielelezo hicho ni glasi ya plastiki rangi ya bluu ambayo ndani yake kulikuwa kuna mabaki ya unga ulioganda uzaniwao kuwa ni sumu” alidai Lowasa, ambaye anatoka katika Kurugenzi ya Huduma na Sayansi Jinai na yupo katika ofisi hizo kwa muda wa miaka saba.

“Pia, nilikagua barua ya maombi ya kufanya uchuguzi kielelezo kilichowasikisha ili kubaini kama kilikuwa na simu na kama, ilikuwa nio sumu ya aina gani na ina madhara gani kwa binadamu,” amedai.


Alidai, pia jeshi la polisi waliomba kufahamu kama unga huo ulichangwa na kimiminika cha aina gani.

“Nilianza kufanya uchunguzi kwa kuchukua sambuli na moja moja kwa kutumia mtambo na nyingine kwa kutumia maji ya maabara. Baada ya kukamilisha uchunguzi huo, Oktoba 31, 2024 aliandaa taarifa ya uchunguzi na kusaini na kisha kuvifunga kwa kutumia lakili kielelezo hicho.”

Hata hivyo, shahidi huyo alidai kuwa kielelezo hicho alikihifadhi hadi Aprili 22, 2026, alipokileta mahakamani hapo, baada ya kuandikiwa barua na Ally Kweka, akiombwa akipelekea kielelezo mahakamani hapo.

Hata hivyo, kielelezo hicho ripoti ya uchunguzi  vimepokelewa na mahakama hiyo na kuwa sehemu ya ushahidi katika kesi hiyo.

Alipoulizwa na wakili Massawe matokeo ya uchunguzi wake yalibainisha nini? Shahidi huyo alidai kuwa unga huo ulioganda ndani ya glasi (bilauli) ya plastiki ulikuwa ni mchangayiko wa aina mbili za dawa za binadamu na mmoja kati ya dawa hizo hutumika kutibu magonjwa ya afya ya akili na nyingine hutumika kutibu magonjwa ya kuhara.

“Katika uchunguzi wa sampuli niliyoufanya, nilibaini mchanganyiko ule ulikuwa ni wa dawa aina mbili ambazo ni Chlorpromazine inayotumika  kutibu magonjwa ya afya ya akili na Metronidazole(flagyl) ambayo hutibu magonjwa ya kuraha”alidai

Aliendelea kudai kuwa alitumia pia kazi data ili kujua madhara wa mtu anayetumia dawa hizo.

“Madhara ya mchanganyiko wa dawa hizo zikitumika kwa wingi zinaweza kusababisha kifo kwa mtumiaji na hii inategemea na kiasi alichotumia” alidai .

Shahidi huyo ambaye majukumu yake ya kazi ni kupokea na kufanya uchunguzi wa vielelezo na sampuli mbalimbali zinazohusiana na makosa ya jinai, kama vile vielelezo vya dawa za kulevya, vyakula, mazingira, ukaguzi wa kemikali pamoja na kutoa ushahidi Mahakamani alidai mafunzo yake aliyapata Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM) mwaka 2016 ambapo alipata shahidi ya kwanza ya Kemia.

Baada ya kutoa ushahidi wake, aliulizwa maswali ya dodoso na wakili wa utetezi, Roman Lamwai na sehemu ya maswali hayo ilikuwa kama ifuatavyo.

Wakili:- Shahidi kwa kazi yako unaweza kupima vipimo vya DNA, ni kweli au si kweli?


Shahidi:- Ni kweli

Wakili:- Ni kweli hujaleta hapa mahakamani barua uliletewa na Polisi kwa ajili ya kufanya uchunguzi?

Shahidi:- Ni kweli Sijaileta

Wakili:- Katika uchunguzi wa sambuli za unga uliokuwepo ndani ya glasi ya plastiki, ulituambia unga huo una wingi kiasi gani?

Shahidi:- Sikupima

Wakili:- Kwa utaratibu wa ofisi yako,  sumu au maji maji unaweza kupima yakiwa katika mwili wa mtu?

Shahidi:- Ndio

Wakili:- Unapima kwa kutumia nini?

Shahidi:- Damu au mkojo

Wakili:- Je uliwahi kuletewa damu au mkojo upime kuhusiana kielelezo hicho?

Shahidi:- Sikuletewa