Moto wateketeza maduka sita Moshi
Watu wakiokoa baadhi ya bidhaa baada ya maduka sita kuteketea kwa moto katika mji mdogo wa Himo mkoani Kilimanjaro. Picha na Mtandao
Muktasari:
Maduka sita yameteketea kwa moto eneo la njia panda katika mji mdogo wa Himo wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro.
Moshi. Maduka sita yameteketea kwa moto eneo la njia panda katika mji mdogo wa Himo wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumapili Juni 27, 2021 Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani humo, Inspekta Abraham Ntezidyo amethibitisha kuungua kwa maduka hayo na kwamba wanaendelea kuchunguza chanzo cha moto huo.
Mmoja wa wafanyabiashara walionguliwa na maduka, Eliaichi Mrema amesema maduka yote sita yameteketea kwa moto huku na kwamba vitu vichache ndio vimeokolewa.
"Mchana kulikuwa na tatizo la umeme kukatika mara kwa mara, muda mfupi baadaye wakati narudi kutoka kanisani nikakuta duka langu linaungua moto, eneo nilipo maduka yote sita ikiwemo la dawa za binadamu, magodoro na mengine yote yameungua."
"Gari la Zimamoto lilifika kwa kuchelewa na vitu vichache tu ndio vimeokolewa kama magodoro vingine vyote vimetejetea kwa moto," amesema Eliaichi.