Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Msigwa, Mbowe watinga kortini Mbeya

Muktasari:

Mshtakiwa mwingine ni Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.

Mbeya. Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe wamefika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya kufuatilia kesi inayomkabili mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi.

Mbunge huyo maarufu kwa jina la Sugu na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga wanashtakiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.

Wawili hao wanadaiwa kutenda kosa hilo Desemba 30,2017 katika mkutano wa hadhara walioufanya kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge.

Kesi hiyo inaendelea leo Alhamisi Januari 25,2018 kwa washtakiwa kutoa ushahidi.

Washtakiwa wanawakilishwa na mawakili Boniface Mwabukusi, Hekima Mwasipu na Sabina Yongo.

Kesi hiyo inasikilizwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Michael Mteite.