Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtanzania aibuka kidedea mashindano ya Quran Afrika

Mtanzania Ahmed Salim

Muktasari:

  • Mtanzania Ahmed Salim ameibuka kidedea baada ya kuwa mshindi wa kwanza katika kipengele cha Tajweed kwenye mashindano ya Quran Afrika yaliyofanyika jana Jumapili Agosti 14, 2022 jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam. Mtanzania Ahmed Salim ameibuka kidedea baada ya kuwa mshindi wa kwanza katika kipengele cha Tajweed kwenye mashindano ya Quran Afrika yaliyofanyika jana Jumapili Agosti 14, 2022 jijini Dar es Salaam.

Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Wanazuoni wa Afrika ya Muhammad wa sita ya nchini Morocco, yalikuwa na washiriki 88 kutoka nchi 34 katika bara la Afrika.

Nafasi ya pili katika kipengele hicho ilichukuliwa na Omar Toure kutoka Guinea na ya tatu imekwenda kwa Abdulsami Hussein kutoka Somalia.

Pamoja na Ahmed kuibuka kidedea katika Tajweed, Binti wa kitanzania mwenye miaka 14, Salma Hassan ameshika nafasi ya tatu katika upande wa Tartil.

Katika mahojiano na waandishi wa habari baada ya kutangazwa mshindi Ahmed amesema haikuwa rahisi yeye kuibuka mshindi kutokana na ugumu wa mashindano.

"Mashindano yalikuwa magumu sana kutokana na kila alieshiriki kufanya vizuri lakini namshkuru Mungu mimi kuongoza," amesema.

Pia, amezishukuru taasisi zilizoshirikiana kuandaa mashindano hayo kwani yanasaidia kuhamasisha vijana kusoma na kuhifadhi kitabu cha Mwenyezi Mungu.

Mashindano hayo yalifanyika kwa takribani siku nne kuanzia Agosti 11 hadi 14 katika msikiti wa Mfalme wa Morocco uliopo makao Makuu ya Bakwata Taifa na kuhudhuriwa na wageni takriban 3,000 kutoka nchi 34 Afrika.

Mgeni rasmi katika mashindano hayo alikuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa akimwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan.