Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtoto atunukiwa zawadi ya kusafiri kwa ndege maisha yake yote

Muktasari:

Mhudumu mmoja wa ndege, ambaye alikuwa amepata mafunzo ya uuguzi alimsaidia mama kujifungua mtoto wakati ndege hiyo ikiwa umbali wa futi 35,000 angani.

India. Shirika la ndege la binafsi nchini India limemtunuku safari za bure mtoto aliyezaliwa ndani ya ndege moja ya shirika hilo iliyokuwa safarini kutoka Saudi Arabia kuelekea India.

Mhudumu mmoja wa ndege, ambaye alikuwa amepata mafunzo ya uuguzi alimsaidia mama kujifungua mtoto wakati ndege hiyo ikiwa umbali wa futi 35,000 angani.

 Kutokana na tukio hilo, shirika hilo lilimpa zawadi ya kudumu maishani, ambayo itakuwa ni kusafiri bure kwa ndege ya shirika hilo katika maisha yake yote.

Mama na mtoto wake walipelekwa hospitalini baada ya ndege hiyo aina ya Boeng 737 kutua katika mji wa magharibi ya Mumbai.

Shirika hilo liliiambia BBC kuwa mama na mtoto wake walikuwa katika afya nzuri.

Kampuni iliwashukuru wahudumu kwa kumsadia mama kujifungua salama.

Shirika hilo lilisema kuwa hiyo ni mara ya kwanza mtoto kuzaliwa kwenye ndege zake.

Tukio kama hilo lilitokea nchini Uturuki ambapo mtoto wa kike alizaliwa katika ndege ya Shirika la Turkey Airline, Aprili mwaka huu.