Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mume amuua mke kisa wivu wa mapenzi

Mume amuua mke kisa wivu wa mapenzi

Muktasari:

  • Mwanamke mmoja mkazi wa kijiji cha Ngulu, wilayani Mwanga, Kilimanjaro, Mwanaidi Hamisi amefariki dunia akidaiwa kukatwakatwa na panga sehemu mbalimbali za mwili wake kutokana na wivu wa mapenzi.


Mwanga. Mwanamke mmoja mkazi wa kijiji cha Ngulu, wilayani Mwanga, Kilimanjaro, Mwanaidi Hamisi amefariki dunia akidaiwa kukatwakatwa na panga sehemu mbalimbali za mwili wake kutokana na wivu wa mapenzi.

Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Abdallah Mwaipaya amesema tukio hilo limetokea Septemba 17, 2021 Kata ya Kwakoa.

Amesema wanandoa hao walikuwa wametengana kwa muda na Septemba 16 mwanaume huyo alimuomba mkewe watoke pamoja kujivinjari.

"Hawa wanandoa walikuwa wametengana kwa muda, juzi mwanaume akamwomba mkewe watoke ambapo alikubali ilipofika jioni mwanaume akamwomba arudi naye nyumbani kwake mwanamke akaridhia," amesema.

"Kumbe mwanaume alikuwa na nia ovu alipofika nyumbani akaanza kumkatakata kwa kutumia panga sehemu mbalimbali za mwili wake na baada ya kutenda tukio hilo alitoweka,"amesema Mwaipaya.

Mwaipaya amesema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini chanzo cha mauaji hayo.

Mwili wa mwanamke huyo umehifadhiwa katika hospitali ya Wilaya ya Same kwa taratibu za mazishi.