Muuguzi anayedaiwa kumbaka mjamzito asimamishwa kazi
Muktasari:
Emmanuel Mpanduji, muuguzi wa zahanati ya kijiji cha Luganga wilayani Mbogwe Mkoa wa Geita anayedaiwa kumbaka mjamzito amesimamishwa kazi.
Mbogwe. Emmanuel Mpanduji, muuguzi wa zahanati ya kijiji cha Luganga wilayani Mbogwe Mkoa wa Geita anayedaiwa kumbaka mjamzito amesimamishwa kazi.
Akizungumza leo Alhamisi Januari 23, 2020 kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Samwel Makala amesema amefikia uamuzi wa kumsimamisha kazi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake.
Muuguzi huyo yupo rumande baada ya kusomewa mashtaka ya kubaka katika mahakama ya wilaya ya Mbogwe na kukosa dhamana.
“Tayari tumemsimamisha kazi wakati kesi yake ikiendelea mahakamani na uchuguzi zaidi unafanyika,” amesema.