Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Muwasa: Upungufu wa umeme chanzo kukosekana maji Moshi

Muktasari:

  • Akitoa maelezo katika kikao cha baraza la madiwani wa manispaa hiyo kilichofanyika leo Ijumaa Novemba 3, 2023; Florah Nguma, Ofisa Uhusiano wa Muwsa, amekiri kuwepo kwa tatizo hilo la maji katika eneo hilo.

Moshi. Mamalaka ya Maji Safi na Usafi Mazingira Moshi (Muwsa), imesema kuwa changamono ya ukopungufu wa umeme, ni kiini cha zaidi ya kaya 30, katika Mtaa wa Kitandu, Kata ya Longuo B, Manispaa ya Moshi, kukosa huduma ya maji.

Akitoa maelezo katika kikao cha baraza la madiwani wa manispaa hiyo kilichofanyika leo Ijumaa Novemba 3, 2023; Florah Nguma, Ofisa Uhusiano wa Muwsa, amekiri kuwepo kwa tatizo hilo la maji katika eneo hilo.

Awali katika kipindi cha maswali na majibu, Diwani wa kata hiyo, Benedictory Mwashambwa alitaka kujua nini wananchi katika mtaa huo wataondokana na tatizo la ukosefu wa maji kwa zaidi ya miezi miwili, hali inayotishia usalama wa afya zao.

"Kumekuwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji, takribani kaya 30, taasisi za dini na baadhi ya shule za msingi hazijapata maji kwa miezi miwili...tunataka mtuambie ni lini wananchi hawa watapata huduma ya maji kama wananchi wengine," amehoji diwani huyo

Ndipo Nguma, alikiri kuwepo kwa tatizo hilo la maji na kusema linatokana na changamoto ya nishati ya umeme.

"Tumekuwa na changamoto ya upatikanaji wa nishati ya umeme na kwamba hakuna ratiba maalumu ya upatikanaji wake, hii imepelekea adha kubwa ya wananchi kukosa maji, hivyo Mamlaka imebuni mradi mwingine kupitia chanzo cha mserereko ambayo yatatoka katika chanzo cha Rupanga na hivyo itapunguza changamoto hii," amesema.

Amesema utekelezaji wa mradi huo utaanza katika kipindi hiki cha robo ya tatu ya mwaka 2023/24 kupitia mapato ya ndani yenye thamani ya zaidi ya Sh400 milioni na kwamba mradi huo utatekelezwa kupitia wataalam wa ndani ili kumaliza changamoto hiyo.

Nguma amewataka wananchi katika kipindi hiki cha changamoto ya maji wanunue vyombo vya kuhifadhia maji ili kuondokana na changamoto zinazoweza kujitokeza katika kipindi hicho.

Ester Kawau, mmoja wa wananchi waliozungumza kwa nyakati tofauti na Mwananchi Digital, amesema kutokana na tatizo hilo la maji, inawalazimu, kusaka maji umbali mrefu.

"Unakuta mtu una familia kubwa na maji yanahitajika mengi, tunapata usumbufu mkubwa, tunaomba Muwsa waangalie namna ya kutusaidia, ili kumaliza tatizo hili," amesema mkazi huyo wa Kata ya Kata ya Longuo B

Josephat Lyimo, mkazi wa Mtaa wa Kitandu amesema kukosekana kwa maji katika maeneo hayo kunawagharimu ambapo wakati mwingine wanalazimika kununua maji kutoka maeneo mengine ambapo ni gharama.