Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mvua yaleta kizaa zaa Kilimanjaro, wanane wakinusurika 

Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani Kilimanjaro, Charles  Meliyo akiwa ametoka kumuokoa mtoto aliyekuwa amekwama ndani ya nyumba baada ya maji kuzingira katika nyumba waliyokuwa wakiishi katika Kijiji cha Koboko kusini, wilaya ya Siha, Mkoa wa Kilimanjaro.

Muktasari:

  • Mafuriko hayo yametokea leo asubuhi Aprili 11, 2026 katika Kijiji cha Koboko Kusini, Kata ya Nasai, Wilaya ya Siha, mkoani Kilimanjaro ambapo kaya nne zenye watu nane ambazo zimezingirwa na maji zimeokolewa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani humo.

Siha. Watu wanane wamenusurika kusombwa na mafuriko katika Kijiji cha Koboko Kusini, kata ya Nasai, Wilaya ya Siha, mkoani Kilimanjaro baada ya nyumba zao kuzingirwa na mafuriko yaliyotokana na mvua zinazonyesha katika maeneo mbalimbali wilayani humo.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani humo, Jeremiah Mkomagi amethibitisha kuokolewa kwa watu hao ambapo amesema mafuriko hayo yametokea leo Jumamosi asubuhi Aprili 11, 2026 wilayani humo, kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha wilayani humo.

Mafuriko yakiwa yamezingira katika mkazi ya wananchi katika Kijiji cha Koboko kusini, kata ya Nasai, Wilaya ya Siha, Mkoani Kilimanjaro

"Leo Aprili 11 2026 saa 07:45 asubuhi Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kituo cha Siha tulipokea taarifa ya tukio la maji kuzingira katika makazi ya watu (mafuriko) katika Kijiji cha Koboko kusini, Kata ya Nasai, ambapo tulifika mara moja eneo la tukio na kukuta mafuriko yamezingira makazi ya watu," amesema Kamanda Mkomagi.

Kamanda Mkomagi amesema, baada ya kufika eneo la tukio askari wa jeshi hilo, walianza kazi ya kuwatoa watu waliozingirwa na maji ndani ambapo walifanikiwa kuwaokoa watu nane wakiwemo watoto sita na watu wazima wawili ambao walikuwa wamekwama ndani ya nyumba zao kutokana na mafuriko hayo.

Askari wa Jeshi la  Zimamoto na Uokoaji Mkoani Kilimanjaro, Joseph Kanuya pamoja na Charles Meliyo wakisaidiana  kumtoa ndani ya nyumba  mwanamke mmoja ambaye nyumba yake imezingirwa na mafuriko katika Kijiji cha Koboko Kusini kata ya Nasai, Wilaya ya Siha Mkoani Kilimanjaro.

Aidha, Kamanda Mkomagi amesema katika tukio hilo hakuna vifo wala majeruhi na kwamba vitu vilivyokuwemo ndani ikiwemo magodoro, vyombo vya kupikia, majiko pamoja na vifaa vingine vimeharibiwa na mafuriko hayo.

"Jeshi limefanikiwa kuokoa jumla ya watu nane wakiwemo watu wazima wawili, wote Jinsia ya kike pamoja na watoto sita ambao wote ni jinsia ya kike, ambapo idadi kamili ya kaya zillifanikiwa kuokolewa ni jumla ya kaya nne," amesema Kamanda Mkomagi.

Aidha, amesema chanzo cha mafuriko hayo ni kutokana na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo na kusababisha maji kuingia katika makazi ya wananachi.