Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwanamke akutwa amejinyonga Kilimanjaro

Mwanamke akutwa amejinyonga Kilimanjaro

Muktasari:

  • Maria Sigarai (26) mkazi wa kijiji cha Kwalakamu wilayani Rombo amekutwa amejinyonga  huku mwili wake ukining’inia kwenye mti.

Rombo. Maria Sigarai (26) mkazi wa kijiji cha Kwalakamu wilayani Rombo amekutwa amejinyonga  huku mwili wake ukining’inia kwenye mti.

Tukio hilo limetokea Machi 11, 2021 kwenye moja ya  shamba lililopo karibu na kijiji hicho.

Kaimu Kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Ronald Makona amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba wanaendelea na uchunguzi  wa kifo cha mwanamke huyo aliyeacha mtoto wa umri wa miezi minne.

"Machi 11 mwaka huu katika kijiji cha Kwalakamu kata ya Kitirima tarafa ya Usseri wilayani Rombo alikutwa amefariki baada ya kujinyonga kwenye mti kwa kutumia kamba ya katani.”

"Chanzo cha kujinyonga hakijafahamika na uchunguzi zaidi wa tukio hilo unaendelea, mwili umehifadhiwa katika hospitali ya Karume ,"amesema Kamanda Makona.