Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Naibu Waziri wa Afya ataja wanaosababisha upotevu wa dawa

Dk Mollel awaasa wanaoiba dawa hospitalini

Rombo. Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel amesema kuna upotevu mkubwa wa dawa na fedha nchini unaosababishwa na baadhi ya watumishi wa wasio waadilifu.

Alisema hayo juzi alipokagua vituo vya afya na zahanati zilizojengwa kwa nguvu za wananchi na kutelekezwa bila kuwa na dawa, vitendea kazi wala watumishi wilayani hapa.

“Zaidi ya asilimia 95 ya watumishi wa afya wanafanya kazi vizuri lakini hawa wachache wanafanya mambo ya ajabu. Tunaenda kuwatambua ili tutakapowaadhibu wasije wakaona wanaonewa na wasitafute huruma,” alisema Dk Mollel.

“Ukifuatilia kwenye mfumo unakuta fedha zimeshatolewa lakini dawa hakuna, nitamwomba mfamasia wa Mkoa wa Kilimanjaro na mganga mkuu pamoja na watu wa MSD (Bohari ya Dawa Tanzania) waniletee dawa walizozipeleka kwenye vituo husika ambavyo nimevitembelea na fedha ambazo vituo hivyo vimepewa ili tujue tatizo la dawa liko wapi,” alisema Dk Mollel.

Naibu waziri huyo alisema dawa nyingi zinapotea na tatizo hilo amelishuhudia alipotembela hospitali za mkoani Arusha na kuahidi kuwachukulia hatua wote waliohusika kwa namna moja au nyingine.

Alisema kuna mtandao mkubwa wa dawa zinazoibiwa kidogokidogo na huwezi kujua wala kuona madhara yake kwa haraharaka ndio maana ukienda kituo cha afya unaambiwa hakuna dawa .

“Zinachukuliwa kidogokidogo na wajanja, tumegundua kuna matatizo ya kiuongozi kwamba watu wanavyofikiri na wanavyofanya mambo yao na wanavyosimamaia watu, rasilimali fedha na dawa. Hii ni shida ambayo inanzia kwenye hospitali zetu za Taifa mpaka vituo vya afya kuna shida kubwa kwenye usimamizi,” alisema.

Kinachofanywa sasa, alisema ni kuuzima mtandao huo lakini tahadhali ili ieleweke kwamba Serikali haiwachukii watuishi wa afya bali inathamini kazi kubwa wanayoifanya na ila kuna wachache wanaoharibu.

Wachache hao alisema wanapaswa kufahamu wataadhibiwa kutokana na vitendo vyao vya kuharibu m fumo wa afya uliopo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi wa Rombo walisema changamoto kubwa ni kwa wagonjwa wanaotumia bima ya afya wakienda hospitali za Serikali wanaambiwa hakuna dawa hivyo wakanunue kwenye maduka binafsi.

Basilisa Justine, alisema “licha ya kwamba tuna bima za afya tukienda kwenye hizi hospitali zetu tunaambiwa hakuna dawa. Tunaandikiwa vizuri lakini tunaambiwa tukanunue duka la dawa. “Tunamuomba Rais John Magufuli atusaidie tupate huduma vizuri,” alisema.

Mwananchi mwingine, Gundelina Tarimo mkazi wa Ndueni alisema upuungufu mkubwa wa dawa kwenye hospitali zilizopo mjini hapa hivyo akaiomba Serikali kufanya mpango wa kusambaza dawa za kutosha kukidhi mahitaji yaliyopo.

“Changamoto kubwa ni kwamba hospitali zetu zipo mbali halafu cha kushangaza ukifika hospitali unaambiwa hakuna dawa, nenda kanunue dukani. Tunaomba dawa zipatikane katika hospitali zetu hasa kwa sisi wazee ambao hatujiwezi,” alisema Tarimo.

Vito vingi vya afya pamoja na zahanati nchini havina dawa wala wahudumu wa kutosha.