Nani anayeruhusiwa kupiga kura
Muktasari:
Jumapili Watanzania watapiga kura kumchagua raia wa awamu ya tano, wabunge na madiwani. Watu wenye sifa pekee ndiyo wanaoruhusiwa kushiriki uchaguzi huo katika vituo 65,105 nchini kote. Wenye sifa zifuatazo wasikae majumbani bali wajitokeze vituoni na kupiga kura.
Dar es Salaam. Jumapili Watanzania watapiga kura kumchagua raia wa awamu ya tano, wabunge na madiwani. Watu wenye sifa pekee ndiyo wanaoruhusiwa kushiriki uchaguzi huo katika vituo 65,105 nchini kote. Wenye sifa zifuatazo wasikae majumbani bali wajitokeze vituoni na kupiga kura.
- Raia yoyote wa Tanzania aliyetimiza umri wa miaka 18 ambaye ameandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura na ana kadi ya kupigia kura, iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
- Mkazi wa kawaida wa eneo analotaka kupiga kura.
- Mtu ambaye jina lake limeorodheshwa katika daftari la kudumu la wapiga kura au orodha inayobandikwa katika kituo cha kupigia kura.