Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ngoma bado mbich uchaguzi Madagascar

Muktasari:

  • Aljazeera imeripoti kuwa upigaji kura ulianza vizuri licha ya amri ya kutotoka nje usiku kucha siku moja kabla ya uchaguzi, lakini pia na maandamano ya miezi kadhaa kabla ya uchaguzi, huku ikinukuu taarifa ya Reuters kuwa kulikuwa na usalama wa hali ya chini katika Mji Mkuu wa Antananarivo, na kwamba wapiga kura walikuwa wachache.

Dar es Salaam. Upigaji kura nchini Madagascar umekamilika katika uchaguzi wa Rais nchini Madagascar baada ya kipindi kigumu cha kampeni ambapo upinzania umesusia uchaguzi ukidai juu ya dosari kadha kuhusina na uchaguzi huo.

Rais Andry Rajoelina, ambaye ni ‘DJ’ wa zamani aliyeingia madarakani kwa mara ya kwanza kwa kuungwa mkono na jeshi mwaka 2009, anatafuta muhula wa pili mfululizo madarakani.

Wapinzani wake wamekuwa wakisema kuwa Rajoelina wakimshutumu kuwa anafaa kuenguliwa kutokana na kile wanachokiita “kufanya mapinduzi ya kitaasisi" ili kumuwezesha kubaki madarakani.

Aljazeera imeripoti kuwa upigaji kura ulianza vizuri licha ya amri ya kutotoka nje usiku kucha siku moja kabla ya uchaguzi, lakini pia na maandamano ya miezi kadhaa kabla ya uchaguzi, huku ikinukuu taarifa ya Reuters kuwa kulikuwa na usalama wa hali ya chini katika Mji Mkuu wa Antananarivo, na kwamba wapiga kura walikuwa wachache.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa katika maeneo yanamuunga mkono Rajoelina, watu walipanga foleni katika vituo vya kupigia kura, huku katika maeneo ya vitongoji vya upinzani yakiwa wengi tupu, kufuatia Wagombea 10 kutoa wito kwa wapiga kura kususia uchaguzi huo.

Karibu kila siku, wapinzani hao waliitisha maandamano katika Mji Mkuu huo wa Antananarivo huku polisi wakiwatawanya kwa gesi kutumia mabomu ya machozi huku wakiwakamata waandamanaji kadhaa.

"Tunatoa wito kwa kila mtu kutopiga kura. Masharti ya uchaguzi wa ŕais wa uwazi, unaokubaliwa na wote, haujafikiwa,” alisema Roland Ratsiraka, mmoja wa wagombea waliokuwa wakiandamana, wiki hii; huku akiongeza kusema kuwa "Hatutaki kushiriki katika udanganyifu huu, ni mzaha kwa Madagascar."

Rais anayetetea nafasi yake Rajoelina amepuuzia ukosoaji huku huku akiielezea imani yake na matuamaini ya kuchaguliwa tena katika duru ya kwanza ya upigaji kura, huku akiwaonya wapinzani wake kuwa kutothubutu kuzuia watu kupiga kura kwani ni kinyume cha sheria.

"Watu wachache walijaribu kuzuia raia kuelezea chaguo lao. Wana haki ya kutoshiriki lakini idadi ya watu ina haki na wajibu wa kupiga kura,” amesema Rajoelina baada ya kupiga kura katika kitongoji cha Kaskazini mwa Antananarivo cha Atmobe, akiwa ameambatana na mkewe pamoja na watoto.

Utata wa kuchaguliwa tena

Madagascar imekuwa na msukosuko tangu ripoti za vyombo vya habari mwezi Juni kufichua kuwa Rajoelina aliomba na kupewa uraia wa Ufaransa mwaka 2014.

Chini ya sheria za nchi hiyo, ikiwa ni kweli kuwa Rais Rajoelina ana uraia wa Ufaransa, basi alipaswa kupoteza uraia wake wa Madagaska, na pamoja na hayo, wapinzani wake pia walmehioji uwezo wake wa kuongoza nchi.

Hat hivyo, Rajoelina amekanusha kujaribu kuficha uraia wake, akisema kuwa aliamua kupata uraia wa ufaransa ili watoto wake waweze kuendelea na masomo nje ya nchi na kwamba hajawahi kuarifiwa kuhusu kupoteza uraia wake wa Madagascar.

"Sheria iko wazi, lakini hakuna anayechukua jukumu la kuitumia ipasavyo," amesema William Rasoanaivo, anayejulikana kama POV, mchora katuni wa kisiasa aliyeshinda tuzo nchini Mauritius.

Hata hivyo, wapinzani wa Rajoelina wamekasirishwa zaidi na uamuzi ambao umemruhusu mshirika wa karibu na Rais huyo, kuliongoza taifa hilo kwa muda, baada ya Rajoelina kujiuzulu kwa mujibu wa katiba ili kugombea tena urais, Pia wamelalamikia ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi.

"Watu wametambua udikteta tunaoishi chini yake," amesema mkazi wa Madagascar Chrishani Andrianono (55), akilalamikia mafanikio machache ambayo yamepatikana chini ya utawala wa miaka 11 wa Rajoelina na kusemea "hatuoni alichotufanyia."

Wakazi wengine wamesema walikuwa na wasiwasi juu ya changamoto za kiuchumi katika nchi ambayo ni moja ya nchi maskini zaidi duniani.

"Kilicho muhimu kwetu ni kwanza kabisa ni kupata maisha kila siku," alisema Benedicte Lalaoarison, muuzaji wa chupi mwenye umri wa miaka 61 katika soko la Analakely katikati mwa Antananarivo.

Rajoelina ambaye aliingia madarakani kwa mara ya kwanza mwaka wa 2009 baada ya mapinduzi, kisha  kurejea katika uchaguzi wa mwaka 2018 – amekuwa akipuuzia malamiko dhidi yake.

Pale ambao wapinzani wake waliposusia kufanya kampeni, yeye alitumia ndege ya kibinafsi, kifika maeneo mbalimbali ya nchi huku akionyesha shule, barabara na hospitali zilizojengwa wakati wa uongozi wake.

Kampeni yake ililaani wale wanaotaka kususia, akiwashutumu kwa kujaribu "kuhujumu" kura na kuwliweka taifa "mateka".

"Si kuwajibika kuhimiza wapiga kura kutopiga kura," alisema msemaji wa kampeni ya Rajoelina Lalatiana Rakotondrazafy.

Watu milioni 11 wamejiandikisha kupiga kura katika nchi hiyo yenye takriban milioni 30, hata hivyo, uchaguzi huo umekubwa na ususiaji mkubwa.

Upinzani ulisema katika taarifa yake kwamba kiwango cha ushiriki kilikuwa "cha chini zaidi katika historia nzima ya Madagaska" ikitoa takwimu za muda kutoka kwa waangalizi wa uchaguzi.

"Tunathibitisha kwamba mapambano yanaendelea na hatutasimama hadi ushindi upatikane," ilisema taarifa hiyo, kwa mujibu wa Reuters.

Chombo cha uchaguzi CENI kilisema bado hakina takwimu rasmi na hakiwezi kutoa maoni yoyote.

Taifa hilo linaloongoza kwa uzalishaji wa vanila duniani, limekuwa likipambana na umaskini kwani robo tatu ya watu wakiishi katika hali duni, huku likitikiswa na mizozo ya kisiasa iliyoanza mara baada ya uhuru wake kutoka kwa Ufaransa 1960.