Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Odinga ainanga IEBC, uchaguzi wa marudio ukiendelea

Raila Odinga

Muktasari:

  • Mgombea urais wa tiketi ya Azimio la Umoja, Raila Odinga ameeleza kutoridhishwa kwake na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), akidai kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo, Wafula Chebukati alikula njama kuwahujumu.


S:

Mwandishi wetu

Dar es Salaam. Wakati Kaunti za Kakamega na Mombasa zikifanya uchaguzi mdogo wa kuwachagua magavana leo Agosti 29, 2022 bado aliyekuwa mgombea urais wa tiketi ya Azimio la Umoja, Raila Odinga haridhishwi na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ya Kenya inayosimamia uchaguzi huo.

Waziri mkuu mstaafu huyo amesema hayo wakati akizungumza na Wajumbe wa Azimio la Umoja kwenye ziara yake ya Mombasa iliyolenga kumnadi mgombea ugavana wa Azimio la Umoja, AbdulSwamad Nassir.

"Wafula Chebukati aliwafanyia vitendo visivyo vya kiungwana makamishna wake waliokataa kusimama upande usio wa kweli.

“Inatakiwa ajitoe kusimamia uchaguzi wa hapa Mombasa kwasababu amekosa sifa na Imani ya watu," Raila amemtuhumu Chebukati.

Uchaguzi huo unafanyika ikiwa ni baada ya uchaguzi wa awali uliotakiwa kufanyika Agosti 9, 2022 kukumbwa na kasoro kwenye maeneo hayo ikiwemo pamoja na kuchanganyika kwa makaratasi ya kupigia kura.

Hali hii inatokea wakati Tume hiyo ikiwa imegawanyika sehemu mbili huku upande wa kwanza ukiongozwa na Mwenyekiti Wafula Chebukati na makamishina wawili huku upande wapili ukiongozwa na Makamu Mwenyekiti, Juliana Cherera na makamishna wengine watatu.

Chanzo cha kutengana huko ni kutokubaliana na matokeo ya urais yaliyotangazwa na tume hiyo Agostiu 15, 2022.

Hata hivyo, wakati kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi iliyofunguliwa na Raila Odinga ikiendelea katika mahakama ya juu ya Milimani nchini humo, upande wa IEBC umedhamilia kuweka mawakili 26 kwa ajili ya kuisimamia kesi hiyo.