Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

OUT yaiangukia Serikali deni la malipo ya watumishi

Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania, Mizengo Pinda akimtunuku mmoja wa wanafunzi wa shahada ya uzamivu katika mahafali ya 43 ya Chuo Kikuu Huria yaliyofanyika mjini Kigoma, leo Desemba 5,2024

Muktasari:

  • Chuo Kikuu Huria Tanzania, kimeomba Serikali kuingilia kati ulipwaji deni la Sh5.3 bilioni ikiwa ni shahiki za watumishi wa chuo hicho kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2020 hadi 2022.

Kigoma. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kimeiomba Serikali kuharakisha ulipaji wa deni la Sh5.3 bilioni kwa wafanyakazi wa chuo hicho kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia Julai 2020 hadi Juni, 2022 ikiwa ni stahiki zao za kiutumishi ikiwepo posho za nyumba na madaraka.

Hayo yamebainishwa leo Desemba 5, 2024 kwenye mahafali ya 43 ya chuo hicho ambapo kitaifa yamefanyika mjini Kigoma na wahitimu 4,307 walihitimu ngazi mbalimbali za elimu, Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Elifas Bisanda amesema deni hilo limeshahakikiwa lakini bado halijalipwa kutoka hazina.

Profesa Bisandi amesema deni hilo limekuwa changamoto kwao na kuwafanya watumishi wa chuo hicho kuwa na hali mbaya sana hasa wale wanaostaafu kutokupewa stahiki zao hivyo kuomba serikali kuingilia kati deni hilo liwezwe kulipwa.

“Kutokulipwa kwa stahiki zetu kama watumishi tumekuwa na hali mbaya na ngumu kwa kipindi hichi hasa kwa wastaafu hivyo tunaomba Serikali iweze kuingilia kati na kutusaidia ili tuweze kupata kwa wakati,”amesema Profesa Bisanda.

 Akizungumza katika mahafali hiyo Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka wahitimu wa vyuo vikuu nchini kutumia taaluma zinazotolewa vyuoni, kama fursa ya kuendeleza Taifa kiuchumi, kwa kufanya tafiti zenye tija, sambamba na kusaidia kuvumbua viwanda hasa katika sekta ya kilimo na kunufaisha watanzania wa hali ya chini.

“Chuo kiongeze juhudi za kuwafikia wanafunzi wengi zaidi kwa Afrika Mashariki na Afrika yote kwa ujumla kwa kuandaa kozi zenye ubora zitakazowashawishi kujiunga na chuo hicho na kufanya utafiti ili kujua dunia inataka nini kwa sasa,”amesema Waziri Mkuu.

 Akitoa salamu za Mkoa wa Kigoma, Mkuu wa Mkoa wa huo, Thobias Andengenye amesema kufanyika kwa mahafali hayo mkoani humo ni sehemu ya mkakati wa Serikali kufungua uchumi wa Mkoa wa Kigoma na kuwa mkoa wa kimkakati kwenye maswala la uchumi na biashara.

“Nichukue nafasi ya kuwakaribisha wote ikiwemo wahitimu wa leo kuja kuwekeza katika mkoa wetu wa Kigoma, kama ambavyo mnaona tunayo mvua ya kutosha, ardhi ya kutosha na ni lango la biashara kwa upande wa Magharibi kutokana na jiografia yetu ya kupakana na nchi jirani ya Burundi, Rwanda, Zambia na Demokrasia ya Jamhuri ya Congo (DRC),” amesema Andengenye.

Akizungumza baada ya kutunukiwa Shahada ya umahiri katika Mawasiliano ya Umma (Master of Arts in Mass Communication), mwandishi mwandamizi wa Gazeti la Mwananchi, Daniel Mjema amesema safari ya kuitafuta ngazi hiyo ya elimu haikuwa lelemama bali ilihitaji nidhamu, kujituma na kuhakikisha mwanafunzi anajiwekea malengo ya kumaliza na kujiwekea mifumo ya kujipima kama yuko ndani ya malengo aliyojiweke.

"OUT ni chuo bora sana cha masafa hapa Afrika ambacho ni wewe mwenyewe utaamua uhitimu kwa wakati au usome masters (shahada ya umahiri) kwa miaka hata sita au zaidi. Ukiingiza uvivu katika kufanya assignment (majaribio) na mitihani unaweza kujikuta unasoma muda mrefu zaidi," amesema Mjema.

"Mie nitoe wito kwa wanahabari tuitafute elimu kwa bidii hasa kupitia OUT ambacho unafanya kazi huku unasoma. Halafu wanahabari tunapaswa kufahamu sheria ya huduma za habari ya 2016 imeweka kiwango cha chini cha elimu kwa mwanahabari. Fursa za kusoma zipo tukiweka nia na malengo," amesisitiza Mjema.

Naye, James Lerombo amehitimu Shahada ya Umahiri wa Uandishi wa Habari amesema elimu hiyo ni chachu katika kuboresha kazi zake na kwamba uwepo wa wasomi kwenye Taifa kunaleta mabadiliko chanya.