Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Petroli, dizeli zashuka bei Oktoba

Muktasari:

  • Bei za mafuta hayo zimeshuka katika mikoa yote Oktoba 2024, ikilinganishwa na Septemba, Ewura imesema bei za soko la Uarabuni ni miongoni mwa sababu.

Dar es Salaam. Bei ya petroli na dizeli ya rejareja kwa Oktoba 2024 imeshuka nchini, ikilinganishwa na Septemba, huku sababu kadhaa zikitajwa, ikiwamo kushuka kwa gharama za soko la Uarabuni.

Taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) inaonyesha bei za mafuta kuanzia leo Jumatano Oktoba 2, 2024 kwa yanayochukuliwa Bandari ya Dar es Salaam, petroli imeshuka kutoka Sh3,140 Septemba kwa lita moja hadi Sh3,011 Oktoba, sawa na asilimia 4.1.

Pia, kwa petroli inayochukuliwa katika Bandari ya Tanga, lita moja imeshuka kutoka Sh3,141 Septemba hadi Sh3,016 Oktoba na kwa Bandari ya Mtwara pia imeshuka kutoka Sh3,142 Septemba hadi Sh3,016 Oktoba.

Kwa upande wa bei ya dizeli, taarifa ya Ewura inaeleza bidhaa hiyo inayopokewa Bandari ya Dar es Salaam bei yake imeshuka kutoka Sh3,011 Septemba hadi Sh2,846 Oktoba.

Dizeli inakayopokewa katika Bandari ya Tanga imeshuka kutoka Sh3,020 Septemba hadi Sh2,859 Oktoba na Bandari ya Mtwara imeshuka kutoka Sh3,021 Septemba hadi Sh2,862 Oktoba kwa lita.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Dk James Mwainyekule, imetaja mwenendo wa bei za mafuta katika soko la Uarabuni kushuka kuwa miongoni mwa sababu za kupungua kwa bei hiyo.

“Bidhaa za mafuta zinazoagizwa na kupokelewa hapa nchini zinazingatia bei za mafuta yaliyosafishwa (FOB) kutoka soko la Uarabuni. Oktoba 2024, bei kikomo za mafuta zimekokotolewa kwa kuzingatia bei za soko la Uarabuni za Septemba 2024.

“Ikilinganishwa na Agosti 2024, bei za zimepungua kwa asilimia 7.42 kwa petroli, asilimia 9.15 kwa dizeli na asilimia 8.23 kwa mafuta ya taa.

Pia, taarifa hiyo imetaja sababu nyingine ni gharama za uagizaji mafuta (Premiums) zimeongezeka kwa wastani wa asilimia 2.63 kwa petroli na kupungua kwa asilimia 16.58 kwa dizeli na asilimia 3.39 kwa mafuta ya taa.

Katika Bandari ya Dar es Salaam; zimeongezeka kwa wastani wa asilimia 11.56 kwa petroli na dizeli katika Bandari ya Tanga; na pia zimeongezeka kwa wastani wa asilimia 9.56 kwa mafuta ya petroli na dizeli katika Bandari ya Mtwara.