Polisi kuchunguza madai askari kugeuza simu za wizi mradi binafsi

Tuesday November 30 2021
POLISICIP
By Mwandishi Wetu

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi nchini limeanza kufanyia kazi habari ya uchunguzi ya gazeti la Mwananchi kuhusu baadhi ya askari wake kugeuza simu za wizi kuwa mradi wao binafsi kwa kuchukua fedha kwa watu waliopoteza au kuibiwa simu.

Katika taarifa yake jeshi hilo limesema, "Jana Novemba  katika  moja ya magazeti ya hapa nchini ilitolewa taarifa yenye kichwa cha habari " Askari wageuza simu za wizi mradi binafsi. Hata  leo Novemba 30 gazeti hilo pia limeandika taarifa nyingine yenye kichwa cha habari 'Mapya yaibuka askari kugeuza simu za wizi mradi binafsi'.

Jeshi la polisi lingependa kutamka kwamba kuanzia jana  taarifa hiyo ilianza kufanyiwa uchunguzi wa kina wa kubaini askari hao wachache wanaofanya vitendo hivyo."

Advertisement