Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Polisi Simiyu wamnasa luteni feki wa JWTZ

Emanuel Mapana mkazi wa mtaa wa Sima mjini Bariadi Mkoa wa Simiyu aliyekamatwa akiwa na sare zinazofanana na za jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ). Picha na Samwel Mwanga

Muktasari:

  • Mtu huyo aliyefahamika kwa jina la Emmanuel Mapana (24), mkazi wa Mtaa wa Sima mjini Bariadi, alikutwa na sare zinazofanana na za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) akiwa na cheo cha luteni.

Simiyu. Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu limemkamata mtu mmoja anayejifanya askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), akiwa na sare za jeshi hilo.

Mtu huyo aliyefahamika kwa jina la Emmanuel Mapana (24), mkazi wa Mtaa wa Sima mjini Bariadi, alikutwa na sare zinazofanana na za jeshi hilo, zikiwa na cheo cha luteni.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP), Edith Swebe, mtuhumiwa amekamatwa na kikosi kazi cha kupambana na uhalifu na wahalifu mkoani humo leo, Ijumaa Februari 14, 2025 saa 6:30 mchana.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa mtuhumiwa amekutwa kwenye gari na baada ya upekuzi amekutwakombati hizo, mkanda wa JWTZ na kompyuta mpakato moja.

Polisi wamesema Mapana alikuwa akitafutwa muda mrefu na jeshi hilo kwa kosa la kujifanya mtumishi wa Serikali.

Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu limetoa wito kwa wananchi wote kuendelea kushirikiana nalo kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu.

Matukio ya watu kukamatwa na sare za majeshi mbalimbali yamekuwa yakijiorudia hapa nchini na kuna kipindi JWTZ iliwahi kutoa kipindi cha msamaha kwa watu walio nayo kuyasalimisha.