Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Polisi wachunguza tukio la majeruhi kushushwa njiani na gari la wagonjwa

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Simon Maigwa.

Muktasari:

  • Tukio lililotokea Mei 6, 2026 katika eneo la Mbwaruki, wilayani Moshi, ambapo mashuhuda walidai kuona gari la wagonjwa (ambulance) hilo likimshusha kijana aliyekuwa katika hali mbaya kiafya kabla ya kuondoka kusikojulikana.

Moshi. Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro limeanza uchunguzi wa tukio la kijana aliyedaiwa kushushwa njiani na gari la wagonjwa (ambulance) kabla ya kufariki dunia, huku likitoa ufafanuzi wa kilichotokea baada ya taarifa hizo kuzua mjadala mkubwa mitandaoni.

Taarifa hiyo inafuatia tukio lililotokea Mei 6, 2026 katika eneo la Mbwaruki, wilayani Moshi, ambapo mashuhuda walidai kuona gari hilo likimshusha kijana aliyekuwa katika hali mbaya kiafya kabla ya kuondoka kusikojulikana.

Akizungumza kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa leo Alhamisi Mei 7, 2026, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amesema mtu huyo ametambulika kuwa Ismail Mbowe (33), mkazi wa Machame.

Kwa mujibu wa Kamanda Maigwa, tukio hilo lilianzia kwenye ajali ya barabarani iliyotokea majira ya saa moja usiku katika eneo la Uchira Karamsingi, ambapo marehemu alikuwa akiendesha pikipiki aina ya Sinoray akitokea Himo kuelekea Moshi Mjini.

Amesema wakati akiendesha pikipiki hiyo, alijaribu kulipita guta lililokuwa mbele yake na kwenda upande wa kulia wa barabara, hali iliyosababisha kugongana na lori aina ya Howo lililokuwa likitokea Moshi kuelekea Njiapanda.

“Ajali hiyo ilisababisha majeraha katika sehemu mbalimbali za mwili wake na wananchi waliokuwa eneo la tukio walitoa msaada wa awali kwa kusimamisha gari lililotajwa kuwa la wagonjwa kwa ajili ya kumpeleka hospitalini,” amesema Kamanda Maigwa.

Amesema majeruhi huyo alikuwa ameambatana na ndugu yake ndani ya gari hilo, lakini wakiwa njiani kuelekea hospitali dereva wa ambulance alisimamisha gari katika eneo la Mbwaruki na kumshusha kabla ya kuondoka bila kumfikisha kituo cha matibabu.

“Jitihada zilifanyika na majeruhi huyo alifikishwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi, ambapo alithibitishwa kufariki dunia,” imeeleza taarifa ya Polisi.

Aidha jeshi hilo, limetoa wito kwa wananchi kutoa taarifa zitakazosaidia kumpata dereva huyo ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.