Polisi yakiri kumshikilia 'Boni Yai', kupekuliwa nyumbani kwake
Dar es Salaam. Jeshi la Polisi limekiri kumshikilia aliyekuwa meya wa zamani wa Ubungo, Boniface Jacob 'Boni Yai', huku likitaka taarifa za kutekwa kwake zipuuzwe.
“Jeshi la Polisi limemkamata na linamshikilia Boniface Jacob, mkazi wa Mbezi kwa Msakuzi, jijini Dar es Salaam kutokana na makosa ya kijinai anayotuhumiwa nayo.
“Hivyo, wananchi wapuuze uongo unaosambazwa mitandaoni kuwa ametekwa,” imeeleza taarifa hiyo iliyotolewa na msemaji wa jeshi hilo, David Misime.
Awali, Mwananchi ilipomtafuta Kamanda wa Polisi wa Kinondoni, Mtatiro Kitwinkwi kujua taarifa za kukamatwa kwa Boni Yai zilizokuwa zikisambaa mitandaoni, alisema “Hapana, sina taarifa.”
Taarifa za Jacob kukamatwa, zimeanza kusambaa mitandaoni dakika chache zilizopita leo Jumatano Septemba 18, 2024 na kwamba amekamatiwa Sinza, jijini Dar es Salaam.
Mwananchi limemtafuta, Wakili wa Chadema, Hekima Mwasipu ambaye amesema Polisi wanakwenda na mteja kwake nyumbani kwake kwa ajili ya kufanya upekuzi.
Endelea kufuatilia Mwananchi