Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pombe haramu zatajwa kuchochea uhalifu Rombo

Pombe haramu zatajwa kuchochea uhalifu Rombo

Muktasari:

Wananchi kada mbalimbali wilayani Rombo wakiwemo wasaidizi wa kisheria, madiwan na wananchi wameeleza namna unywaji wa pombe haramu unavyochangia matukio ya kikatili wilayani humo.

Rombo. Wananchi kada mbalimbali wilayani Rombo wakiwemo wasaidizi wa kisheria, madiwan na wananchi wameeleza namna unywaji wa pombe haramu unavyochangia matukio ya kikatili wilayani humo.

Licha ya elimu kutolewa kwa jamii kupitia vyombo mbalimbali pamoja na viongozi wa dini, matukio ya ukatili yameendelea kuitesa wilaya hiyo ambako haipiti wiki au wiki mbili bila hujasikia mauaji au watoto kubakwa.

Desemba 16 mwaka jana binti wa miaka 11 mkazi wa Kijiji cha Nayeme, alibakwa na mzee wa miaka 55 na kisha kwenda kumtelekeza Mto Tarakea usiku wa manane huku akiwa amefungwa kitambaa mdomoni, mikono na miguu ikifungwa kwenye mti ulioko ndani ya mto huo.

Tukio hili liliibua hisia za watu mbalimbali kufuatia unyama huo huku baadhi yao wakiiomba Serikali kuwakamata na kuwaadhibu vikali watu wanaofanya vitendo vya namna hiyo.

Binti huyo alipotafutwa na gazeti hili alisimulia mwanzo mwisho wa tukio hilo mpaka alivyokutwa mtoni na kuokolewa na msamaria mwema aliyekuwa anapita asubuhi ya Desemba 17.

Anasema kabla ya kupoteza fahamu, alipewa pombe ya kienyeji inayodaiwa kuchanganywa na kilevi kingine na baada ya kunywa hakujitambua.

Hata hivyo, siku chache baada ya tukio hilo kijana mwingine wa miaka 29, Venance Aloyce mkazi wa Kijiji cha Mrere wilayani humo alikutwa ameuawa na mwili wake kukutwa mtupu na ukiwa umetupwa kwenye korongo la Kitovata Mashati.

Akisimulia tukio hilo mama mzazi wa kijana huyo, Mariselina Aloyce alisema mwanae alipoondoka nyumbani Desemba 27 mwaka huu hakurudi nyumbani na kuwa siku iliyofuata msamaria mwema ambaye alipita eneo mwili huo ulipotelekezwa, alimpa taarifa kuwa kuna mwili wa mwanaye umetelekezwa eneo la Kitovata

Kufuatia matukio hayo, Kaimu Kamanda wa polisi Mkoani humo, Ronald Makona alithibitisha kutokea kwa matukio hayo na kusema jeshi hilo linawasaka wale wote waliohusika na matukio hayo ili kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Akizungumzia chanzo cha matukio hayo, Remmy Shirima kutoka shirika lisilo la kiserikali (Ajiso) alisema wamekuwa wakitoa elimu kila mara kwa jamii lakini tatizo kubwa linalowakumba wengi ni ulevi wa kupindukia.