Putin alitaka jeshi la Ukraine kuondoa uongozi wa nchi

Rais wa Russia, Vladimir Putin

Muktasari:

  • Rais wa Russia, Vladimir Putin amelitaka jeshi la Ukraine kuondoa uongozi uliopo madarakani wa Rais Volodymyr Zelensky huku akiutuhumu kuwa wa kigaidi na genge la watumiaji wa dawa za kulevya

Rais wa Russia, Vladimir Putin amelitaka jeshi la Ukraine kuondoa uongozi uliopo madarakani wa Rais Volodymyr Zelensky huku akiutuhumu kuwa wa kigaidi na genge la watumiaji wa dawa za kulevya

Putin amewashtumu raia wa Ukraine kwa kutuma vifaa vya kivita kwenye makazi ya watu na miji mikubwa ikiwamo Moscow hali inayotishia usalama na kuongeza hofu.

Tuhuma hizo huenda zikaleta hali ya hofu huku ikidaiwa kuwa Urusi inazitumia kama sababu ya kuua raia wa Ukraine.

Zaidi ya watu 100 wauawa Ukraine

Ukraine imesema kuwa zaidi ya watu 100 wameuawa hadi sasa katika uvamizi wa Russia, huku mapigano yakienea kote nchini na vikosi vya Russia vikisonga mbele kuelekea mji mkuu, Kyiv. Soma zaidi 

 Zifahamu nguvu za kijeshi Russia na Ukraine

Mashambulizi ya kijeshi ya Russia nchini Ukraine yamewashangaza wengi huku wengine wakitamani kujua nguvu za kijeshi za mataifa hayo ya Ulaya Mashariki ambayo yamekuwa kwenye mgogoro kwa miaka kadhaa.

Takwimu zilizotolewa usiku wa jana na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky zinaonyesha kwamba watu 137 wameuawa kwenye mashambulizi hayo na wengine 316 wakijeruhiwa. Soma zaidi