Rais ateua wajumbe Tume kuboresha haki jinai
Muktasari:
- Rais Samia Suluhu Hassan ameteua wajumbe tisa wa Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuboresha taasisi za Haki Jinai nchini inayoongozwa na Mwenyekiti Jaji Mohamed Othman Chande na Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu Balozi Ombeni Sefue.
Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan ameteua wajumbe wa Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuboresha taasisi za Haki Jinai nchini inayoongozwa na Mwenyekiti Jaji Mohamed Othman Chande na Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu Balozi Ombeni Sefue.
Taarifa iliyotolewa jana Januari 6 na Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunus imewataja wajumbe hao kuwa pampoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Dk Eliezer Feleshi, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais (Utumishi) Dk Laurean Ndumbaro, Mkuu wa Jeshi la Polisi mstaafu Said Mwema na Mkuu wa Jeshi la Polkisi mstaafu Balozi Ernest Mangu.
Wengine ni pamoja na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Dk Edward Hosea, Askari Polisi mstaafu, Saada Makungu, Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco Omar Issa, Ofisa mwandamizi Ofisi ya Rais Baraka Leonard na Mkurugenzi wa Utafiti katika Chuo Kikuu cha Zanzibar na Rais mstaafu wa Chama cha Wanasheria Zanzibar, Yahya Khamisi Hamad.