Rais Musisi wa Botswana aondoka Tanzania

Friday June 11 2021
raisi pic
By Mwandishi Wetu

Dar es salaam. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Libelata Mulamula amesema ujio wa Rais wa Botswana, Mokgweetsi Masisi  nchini ni ishara ya kudumisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

 Balozi Mulamula ameyasema hayo leo Ijumaa Juni 11, 2021 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) alipokuwa akimsindikiza Musisi aliyemaliza ziara yake ya kizazi ya siku mbili nchini.

Amebainisha kuwa nchi hiyo ipo tayari kushirikiana na Tanzania katika nyanja mbalimbali ikiwemo sekta ya uwekezaji na tayari wameshaanza kwa kukitembelea kiwanda cha Bakhressa, siku chache zijazo bidhaa za kampuni hiyo zitafika Botswana.

 “Kutokana na ziara hii mgeni wetu amefurahi na ameshangazwa  kuona Tanzania ina viwanda vikubwa hivi na chenye uwezo mkubwa..., amekubali kufanya biashara na sisi,” amesema Balozi Mulamula.

Advertisement