Rais Samia afanya uteuzi

Thursday September 16 2021
samia pc

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Dk Yamungu Kayandabila kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo (NDC) na Dk Naomi Katunzi kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) kwa kipindi cha miaka mitatu mingine.


Taarifa ya uteuzi wa viongozi hao iliyotolewa leo Alhamisi Septemba 16, 2021 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu imesema, Dk Kayandabila pamoja na uteuzi huo, ni Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).


"Uteuzi huu umeanza rasmi Septemba 14, 2021," imesema taarifa hiyo.

Advertisement