Rais Samia akutana na Tundu Lissu

Rais Samia Suluhu Hassan alipokutana na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu jijini Brussels nchini Ubelgiji.

Muktasari:

Rais Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu.

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu.

Rais Samia akutana na Tundu Lissu

Taarifa iliyotolewa leo Jumatano Februari 16, 2022 na Mkurugenzi Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Zuhura Yunus imesema kuwa mazungumzo hayo yamefanyika jijini Brussels nchini Ubelgiji baada ya Rais Samia kukubali maombi ya Lissu ya kukutana naye na kuzungumza.

Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu walipokutana jijini Brussels nchini Ubelgiji.

“Katika mazungumzo hayo, Rais na Makamu Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu walizungumza masuala mbalimbali yenye maslahi ya ustawi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania” imesema taarifa hiyo