Rais Samia amweka mtegoni Waziri Aweso, ampa siku 60

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Muktasari:

  • Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemuweka mtegoni Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, akiahidi kumzingua iwapo hatafanikisha kupatikana kwa huduma ya maji katika Wilaya ya Tukuyu mkoani Mbeya ndani ya miezi miwili sawa na siku 60.



Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemuweka mtegoni Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akiahidi kumzingua iwapo hatafanikisha kupatikana kwa huduma ya maji katika Wilaya ya Tukuyu mkoani Mbeya ndani ya miezi miwili sawa na siku 60.

Akiwa ziarani mkoani Mbeya leo Jumapili, Agosti 7, 2022 Mkuu huyo wa nchi amemtaka Aweso kuhakikisha maji yanapatikana katika wilaya hiyo kwa kipindi hicho.

“Waziri wa maji amesema hapa ndani ya miezi miwili maji yatapatikana, mwezi wa nane, tisa wa 10 nitatuma watu kuja kuangalia kama maji yanapatikana.

“Kama hayakupatikana waziri amenizingua naye atajua amezinguliwa na nani na hatua za kuzinguana zitakwenda hivyo, labda awe na sababu ya maana moja ambayo atanambia na itaniridhisha kwa nini maji Tukuyu hayakutoka ndani ya miezi hiyo miwili,” amesema.

Hata hivyo, amesema tayari wahandisi wapo katika maeneo ya kazi wilayani humo, kinachopaswa kufanywa ni kuwasimamia ili waifanye kazi hiyo haraka.