Rais Samia apongeza jitihada za Benki ya CRDB kuchangia maendeleo katika jamii

Rais Samia Suluhu Hassan (katikati) akikata utepe kuzindua ofisi ya Maendeleo kata ya Kizimkazi Dimbani na nyumba mbili za madaktari zilizonjengwa kwa ufadhili wa Benki ya CRDB na kugharimu shilingi milioni 300. Wengine pichani ni, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Zanzibar, Haroun Ali Suleiman (watatu kulia), Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Rashid Hadid Rashid (wakwanza kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Dkt. Ally Hussein Laay (wapili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wapili kulia) na Mwenyekiti wa CRDB Bank Foundation, Martin Warioba (wakwanza kulia).

Muktasari:

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amepongeza jitihada zinazofanywa na Benki ya CRDB katika kuchangia maendeleo katika jamii.

Zanzibar. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amepongeza jitihada zinazofanywa na Benki ya CRDB katika kuchangia maendeleo katika jamii.

Rais Samia ametoa pongezi hizo wakati wa kilele cha Tamasha la Kizimkazi alipokuwa akikabidhiwa miradi ya nyumba za madaktari na ofisi za shehia Kizimkazi Dimbani zilizojengwa kwa udhamini wa Benki hiyo.

Akipokea miradi hiyo iliyo gharimu kiasi cha shilingi milioni 300, Rais Samia alisema Serikali inajivunia ushirikiano wa kimaendeleo baina yake na Benki ya CRDB.

Aliongeza kuwa Benki hiyo imekuwa mfano mzuri wa ushirikiano wa sekta binafsi na sekta ya umma (PPP) kwa kufikia malengo yaliyowekwa katika Dira ya Maendeleo ya 2025. “Suala la kuijenga nchi yetu ni wajibu wa kila mmoja wetu na si la serikali peke yake, niwapongeze Benki ya CRDB kwa kujitoa kwenu kutatua changamoto zilizopo katika jamii.

Wajasiriamali wakifuatilia mafunzo ya uendeshaji biashara na elimu ya fedha yaliyoandaliwa na Benki ya CRDB katika Tamasha la Kizimkazi. Wajasiriamali zaidi ya 300 kutoka vijiji vya Kibuteni, Kizimkazi Mkunguni na Kizimkazi Dimbani walihudhuria mafunzo hayo yaliyofanyika katika Skuli ya Sekondari ya Kizimkazi.

Leo hii mmetutoa kimasomaso kwa kutusaidia kuimarisha sekta ya afya na kuhakikisha wananchi wa Kizimkazi Dimbani wanapata huduma bora za kijamii, ama hakika hii ni Benki ya kiza-lendo,” alisema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia alisifu mafanikio ya Tamasha la Kizimkazi kwa mwaka huu 2021 ambalo lililenga katika kuhamasisha jamii kudumi-sha utamaduni na kuongeza ujumuishaji wa kiuchumi kwa wananchi kwa kuonyesha fursa mbalimbali zitokanazo na tamaduni za Kitanzania.

Tamasha hilo lilihusisha mafunzo kwa wajasiriamali zaidi ya 500 juu ya ubunifu wa bidhaa za asili, elimu ya fedha na uendeshaji biashara, pamoja na michezo mbalim-bali ya asili.Pia alieleza kwamba wakati umewadia kwa Watanzania kuacha utamaduni wa kigeni na kujivunia utamaduni wetu. Alitoa rai kwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuwa na mikakati mbalimbali itakayosaidia kutoa elimu juu ya umuhimu wa kuenzi na kulinda utamaduni wa Kitanzania.

Rais Samia alisema jamii pia ina wajibu wa kushiriki kikamilifu katika matamasha ya utamaduni ili kusaidia ukuzaji na uendelezaji wa mfumo wa utamaduni na sanaa katika jamii ya Kitan-zania. “Benki ya CRDB imetuon-yesha kwa mfano kuwa tukiwekeza katika utamaduni wetu tutafungua fursa nyingi za kiuchumi kwa kutengeneza soko kwa bidhaa zetu za asili na Sanaa yetu.

Kupitia Tamasha hili la Kizimkazi niiombe Wizara iweke mikakati ya kuanzisha matamasha ya utamaduni katika kila kanda hii itasaidia kukuza tamaduni za maeneo mbalimbali na kuchochea utalii,” alisisitiza Rais Samia.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema utekelezaji wa miradi hiyo na uandaaji wa Tama-sha hilo la Kizimkazi ambalo zamani lilikuwa likijulikana kama “Kizimkazi Day,” ni mwendelezo wa utekelezaji wa Sera ya Benki hiyo ya uwekezaji katika jamii ambayo inaelekeza asilimia 1 ya faida ya Benki kila mwaka kwa ajili ya kusaidia jamii kupitia programu bunifu za uwezeshaji.

Nsekela alisema Benki hiyo imedhamiria kwa dhati kusaidiana na Serikali kujen-ga uchumi jumuishi na kuwa utamaduni ni moja ya eneo ambalo Taifa likiwekeza vizuri linaweza kusaidia kuongeza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Pato la Taifa kwa ujumla. “Pamoja na vijielezi vingi vya neno utamaduni, sisi Kama Benki ya kizalendo tunaamini kuwa; utamaduni ni ujasiria-mali, utamaduni ni utalii, uta-maduni ni ajira, utamaduni ni uchumi.”Aidha Nsekela alibainisha kuwa Benki hiyo imedhamiria kuweka mchango wake katika pande zote za Muungano na hivyo kuchochea maendeleo ya Taifa.

Akielezea mchango wa Benki hiyo katika kukuza uchumi wa visiwa vya Zanzi-bar, Nsekela alisema katika nusu mwaka 2021 pekee Benki ya CRDB imetoa zaidi ya shi-lingi bilioni 150 kuwezesha sekta mbalimbali za maendeleo ili kuwezesha ajenda ya Serikali ya kujenga Uchumi wa Buluu.

Alimwambia Mheshimiwa Rais, Benki hiyo pia inajivu-nia zaidi kuleta mapinduzi makubwa katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali ya Map-induzi ya Zanzibar. Mwaka 2014 Benki ya CRDB iliunganisha mfumo wake wa kielekro-niki wa ukusanyaji mapato na mfumo wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar, ambapo ndani ya mwaka mmoja tu makusanyo yaliongezeka kwa zaidi 600%,” aliongezea.

Nsekela alimuahidi Mheshimiwa Rais kuwa Benki ya CRDB kupitia kauli mbiu yake ya “Tupo Tayari” itaendelea kushirikiana na Serikali na wadau wengine wa maendelo nchini ili kufikia malengo yaliyowekwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025.

Pamoja na mafunzo ya uja-siriamali yaliyoendeshwa na Benki ya CRDB, Tamasha la Kizimkazi pia lilijumuisha usafi wa mazingira, mashindano ya michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu na pete, kufua na kukuna nazi, rede, karata , bao, kuvuta kamba, resi za baskeli, resi za ngalawa, shomooo , na mashindano ya kuhifadhi Qurani.

Wananchi pia walipata fursa ya kupata chanjo ya UVIKO 19 ambayo itatolewa katika viwanja vya Kizimkazi Dimbani Mji Mpya, zoezi ambalo liliongozwa na Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mh. Ahmed Nassor Mazrui.

Kilele cha Tamasha la Kizimkazi kilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zan-zibar.

Kuhusu Benki ya CRDB

Benki ya CRDB ni moja ya benki zinazoongoza katika ukanda wa Afrika Mashariki, inatoa huduma kwa wateja wadogo, wakati na wakubwa ikiwamo huduma kwa wateja binafsi, huduma za hazina, huduma za bima, mikopo ya biashara, kilimo na uwezeshaji kwa wajasiriamali wadogo.

Benki ya CRDB ndio benki ya kwanza nchini Tanzania kutambuliwa na kampuni ya kimataifa ya utafiti ya Moody’s Investors Service kuwa moja kati ya benki 10 imara na salama Afrika katika uwekezaji. Moody’s imeipa Benki ya CRDB daraja la uimara la B1 ambalo ni daraja la juu zaidi kupatikana kwa mabenki na taasisi za fedha katika ukanda wa jangwa la Sahara.

Benki ya CRDB imepata utambuzi wa Mfuko wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa (UN Green Climate Fund) tangu mwaka 2019 na pia imetambuliwa kama benki bora Tanzania na jarida la Global Finance kwa mwaka 2020.

Mke wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi akifungua mafunzo maalum ya siku tatu yaliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa wajasiriamali wakati wa Tamasha la Kizimkazi. Mafunzo hayo yalihusisha wajasiriamali zaidi ya 300 kutoka vijiji vya Kibuteni, Kizimkazi Mkunguni na Kizimkazi Dimbani.

Benki ya CRDB imekuwa kiungo muhimu cha biashara katika nchi za Tanzania na Burundi kwa kuwahudumia wateja zaidi ya Sh3 milioni na kupitia mtandao mpana wa matawi 246, zaidi ya CRDB Wakala 19,000, 550 ATM, mashine za manunuzi 1,800 na Kituo cha Huduma kwa Wateja kinachotoa huduma saa 24/7.

Kuhusu Tamasha la KizimkaziTamasha la Kizimkazi lil-ianzishwa rasmi mwaka 2016 kwa Jina la SAMIA DAY mara baada ya Mhe. Samia Suluhu Hassan kuteuliwa kuwa Mgombea Mwenza wa Mhe. Magufuli, mwezi wa sita 2015.

Wakati huo Mhe. Samia akiwa Mbunge anayemaliza muda wake katika Jimbo la Makunduchi, alifanya ziara ya kuwaaga wanachama wa CCM katika matawi ya Jimbo la Makunduchi.

Ziara hiyo ilimalizikia Tawi la CCM K/Mkunguni ambako yeye alikuwa ni mwanachama. Katika kikao hicho cha kuaga, Wanachama na Wajumbe wa Baraza la Shehia K/Mkunguni walimuomba Mhe. Samia aridhie ili iandaliwe siku maalumu kwa ajili ya kuja kuagwa rasmi katika Tawi lake la CCM.

Sherehe hiyo ilifanyika wiki ya pili ya mwezi wa nane (Agosti) 2015, na kutokana na kufana sana kwa sherehe hizo, Mhe. Samia akashauri basi kila ikifika mwezi wa nane Wanakizimkazi wakutane ili kutafakari Maendeleo yaliyopatikana na Changamoto zilizopo ili kuzipatia ufumbuzi na kuleta Maendeleo yao.Kuanzia mwezi wa nane 2016 sherehe hizo kwa mara ya kwanza zikaitwa Samia Day na kuundwa Kamati Maalumu ya Samia Day ambayo ilisimamia sherehe hiyo ambayo ilikuwa ikifanyika Kizimkazi Mkunguni hadi mwaka 2018, ambapo zilibadilishwa jina na kuitwa Kizimkazi Day, na kuanza kuwashirikisha wananchi kutoka Kizimkazi Dimbani katika baadhi ya michezo na resi za ngalawa.

Kadri miaka ilivyoendelea sherehe iliendelea kukua, na kushirikisha Shehia zaidi zikiwemo Mtende, Kibuteni na Muyuni, kama azma ya mama mwenyewe ya kuwa Tafsiri halisi ya Kizimkazi ni Kibuteni, Kizimkazi Dimbani na Kizim-kazi Mkunguni.