Rais Samia atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu TPA

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Eric Hamissi

Muktasari:

  • Muda mfupi baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuweka wazi kuwa haridhidhwi na kasi ya utendaji wa bandari nchini, ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Eric Hamissi.

Dar es Salaam. Muda mfupi baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuweka wazi kuwa haridhidhwi na kasi ya utendaji wa bandari nchini, ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Eric Hamissi.

Rais Samia ajibu wanaobeza ziara za nje

Taarifa iliyoptolewa leo Jumatatu Julai 4, 2022 na Mkurugenzi Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Zuhura Yunus imesema kuwa nafasi Hamissi inachukuliwa na Plasduce Mbossa ambaye ni Naibu Mkurugenzi Mkuu Wa mamlaka hiyo.

Taarifa ya kutengua uteuzi huo imetolewa muda mfupi baada ya Rais Samia kuweka wazi kuwa haridhishwi na utendaji wa bandari nchini.

Mkuu huyo wa nchi alibainisha kutoridhishwa na utendaji wa bandari wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha Tabora-Isaka iliyofanyika katika Ikulu jijini Dar es Salaam.

“Wale tuliowakabidhi uendeshaji wa bandami zetu wafanye kazi kwa kasi mno siridhishwi kabisa na kasi za bandari” alibainisha Rais Samia huku nakiwataka watendaji wa mamlaka hiyo kuchapa kazi.

“Watu huko nje bandari zinaendeshwa kwa kasi kubwa na biashara zinakuwa kwa kasi kubwa, kupitia bandari zetu sisi bado tuna suasua wawekezaji wanakuja ni kuzungushwa mwanzo mwisho nasema bandari watu wafanye kazi” alisisitiza Rais Samia