Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia azindua chuo cha ufundi Kagera

Rais Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China, Chen Mingjian kuzindua Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma (VETA) kilichopo, Burugo kata ya Nyakato Bukoba Mkoani Kagera leo 13 Oktoba, 2022.

Wengine katika picha ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Waziri wa Elimu, Profesa Adolf Mkenda, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila pamoja na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali.

Muktasari:

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Alhamisi Oktoba 13, 2022 amezindua Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma cha Mkoa wa Kagera kilichojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya China kwa gharama zaidi ya Sh22 bilioni.

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Alhamisi Oktoba 13, 2022 amezindua Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma (VETA) cha Mkoa wa Kagera kilichojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya China kwa gharama zaidi ya Sh22 bilioni.

Chuo hicho ambacho kina ofisi za walimu nane, nyumba tatu za walimu, bweni lenye uwezo wa kuhudumia vijana wa kike 214, na wavulana 116, kina uwezo wa kuchukua vijana 400 wa kozi za muda mrefu na 1,000 wa kozi za muda mfupi.

Pia kina madarasa yatakayohudumia watu 218 kwa pamoja na maktaba yenye uwezo wa kubeba wanafunzi 30 kwa wakati mmoja.