Rais Samia: Wasanii acheni kuparurana

Wednesday June 01 2022
By Emmanuel Mtengwa

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amewataka wasani wa muziki nchini kupendana na kuacha kuparurana ili kuendeleza tasnia hiyo na kuliunganisha Taiafa.

Mkuu huyo wa nchi ametoa rai hiyo wakati wa tamasha la msanii wa muziki wa HipHop, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu la The Dream Concert.

Tamasha hilo limefanyika usiku wa kuamkia leo Jumatano Juni Mosi kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam likiwa ni maalumu kwa mbunge huyo wa zamani wa Mbeya Mjini kuadhimisha miaka 30 kwenye tasnia ya muziki.

Rais Samia ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo amesema kuwa wasanii wana mchango mkubwa akiwataka kuungana kupitia tasnia hiyo kwa kuasidiana ili kuliunganisha Taifa.

Ametoa tahadhari ya kuwa na migogoro ndani ya tasnia hiyo akisema hilo si jambo jema katika maendeleo ya muziki na Taifa.

“Niwaase wasanii kupendana, kushirikiana na kusaidiana, mmekuwa na vita nyingi sana baina yenu, ninyi kwa ninyi, wanamuziki wa makundi mbalimbali, hili si jambo jema, lengo letu viongozi wenu ni kuliunganisha Taifa, mnapogombana watu wa sekta moja taifa halitaungana” amesema

Advertisement

“Kwa kiasi kikubwa wasanii mna mchango mkubwa kwenye kuliunganisha Taifa, kwa hiyo naomba muungane, mshikane na msaidiane ili tuweze kuliunganisha vyema Taifa, amewasihi  

Amewataka kutumia vipaji vyao kufikia malengo na si kuanzisha migogoro.

 “Niseme achene kuparuana, tulizaneni, pendaneni. Achene kuperurana. Kila mtu aonyeshe kipaji chake jinsi Mungu alivyomjalia, kila mtu awe na njia yake ya kufika kule anakotaka kufika kama alivyofanya Joseph hapa (Sugu).”

“Pendaaneni wanamuziki” amesisitiza Rais Samia

Pia, Rais Samia amewata wasanii hao kusimamia maadili wakati wanapofanya kazi zao.

“Nawaomba tusimamiane tulina mila, silka na tamaduni zetu, sio nia yangu kuingilia masuala haya lakini niwasihi wasanii muyaone haya weneyewe kabla Serikali haijaingilia” amesema

SOMA: Rais Samia ataja sababu kushiriki tamasha la Sugu

SOMA ZAIDI:Ana miaka chini ya 18 ni historia ya binti nilikutana naye usiku

Advertisement