Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais wa Iran amtaka Trump kwenye majadiliano

 Rais wa Marekani Donald Trump 

Muktasari:

"Sina masharti yoyote. Ikiwa serikali ya Marekani ina nia, basi tuanze mazungumzo hayo sasa," alisema Rouhani


Tehran, Iran. Rais wa Iran Hassan Rouhani Jumatatu alimpa changamoto Rais wa Marekani Donald Trump akisema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inakaribisha mazungumzo na Marekani “hata sasa".

"Sina masharti yoyote. Ikiwa serikali ya Marekani ina nia, basi tuanze mazungumzo hayo sasa," alisema Rouhani wakati wa mahojiano yaliyorushwa kupitia televisheni ya taifa Jumatatu ikiwa ni saa chache kabla ya Marekani kurejesha vikwazo dhidi ya Iran.

"Ikiwa kuna nia ya kweli, Iran mara zote imekuwa ikikaribisha mdahalo na majadiliano,” alisema Rouhani.

Rais Trump alitangaza Mei kuwa nchi yake itajitoa kwenye makubaliano hayo na mapema Jumatatu alisaini hati maalum ya rais ya kurejesha tena vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Iran.

Awamu ya kwanza ya vikwazo imeanza kutekelezwa Jumanne. Vikwazo hivyo vinahusisha sekta za utengenezaji wa magari na chuma cha pua pamoja na biashara ya vito vya thamani, kwamba kampuni yoyote ya kigeni au taasisi ya kifedha itakayokiuka vikwazo hivyo itaweza kuadhibiwa na Marekani.

Awamu ya pili ya vikwazo itaanza kutekelezwa Novemba mwaka huu na italenga biashara zinazohusu bidhaa za petroli hatua inayolenga kupunguza uuzaji wa mafuta ghafi nje ya nchi ya Iran.

Serikali na makampuni kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo Japan yatalazimika kufanya maamuzi ikiwa zitaendelea kutekeleza makubaliano ya kibiashara na Iran au zitayasitisha.

Iran imepinga vikali hatua hiyo ya Marekani na kutishia kufunga mlango bahari ya Hormuz ambao ni njia kuu ya kusafirisha mafuta.

Mshauri wa Taifa wa masuala ya usalama, John Bolton, alipoulizwa kuhusu utayari wa Iran kwa mazungumzo, alitupilia mbali akisema ni "propaganda" rahisi.

"Hebu tusubiri tuone nini kitatokea au ni propaganda zaidi," alisema Bolton na akaongeza kwamba Trump amekuwa na "mwendelezo" usioyumba kwamba atakuwa tayari kujadiliana na tawala kama vile Korea Kaskazini na Iran.