Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

RC Kagaigai aishukia Sido

RC Kagaigai aishukia Sido

Muktasari:

  • RC Kagaigai ameeleza kutoridhishwa na utendaji wa Sido mkoani Kilimanjaro na kuwataka kuwa wabunifu katika kuliendesha shirika hilo.

Moshi. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai ameonyesha kutoridhishwa na utendaji kazi wa Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo (Sido) mkoani humo huku akiwataka kuwa wabunifu katika kuliendesha shirika hilo.

Akizungumza mwisho wa wiki alipofanya ziara ya kikazi kuangalia shughuli za shirika hilo, Kagagai amesema Sido ya mwaka 1980 ni tofauti na ya sasa kutokana na kuzorota kwake kutokana na kukosekana kwa ubunifu unaoendana na teknolojia ya sasa.

"Nimetembelea hili shirika leo na kuna kitu nimegundua. Ofisi hii haina takwimu zinazoeleweka, naona kama Sido imekufa kwa Mkoa wa Kilimanjaro, naomba mjipange vinginevyo maana naona siyo ile Sido ya Mwaka 1970/80 na hii ninayoioana leo ya mwaka 2021," alisema Kagaigai.

Aidha alisema suala la shirika hilo kujiendesha kwa kutumia kodi pekee haitaweza kulifikisha shirika hilo kwenye malengo yake na kwamba wanapaswa kubuni vyanzo vingine vya kuliendeleza shirika hilo.

"Lazima mfanyae kazi kubwa muwe na nguvu kazi ya kutosha pamoja na wafanyakazi kwasababu hata hii shughuli niliyoioana hapa sioni kama inatosha kujiendeleza nina mashaka nayo, mnahitaji kufanya kazi kubwa na ya ziada ili kuongeza uzalishaji badala ya kutegemea majengo lazima muwe wabunifu," amesema Kagaigai

Awali akitoa taarifa ya maendeleo ya shirika hilo, Kamu eneja wa Sido Mkoa wa Kilimanjaro, Alex Masenene amesema changamoto kubwa wanazokabiliana nazo ni mashine chakavu na nyingine kutofanya kazi katika karakana za shirika hilo pamoja na uhaba wa mtaji wa uendeshwaji na uwekezaji katika kuendeleza shughuli za shirika hilo.