RC Mghwira aeleza wadudu waliovamia kijiji walivyodhibitiwa
Muktasari:
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amesema wadudu wanaodaiwa kuwa ni nzige walioonekana katika kijiji cha Karamandei kata ya Toloha wilayani Mwanga walidhibitiwa.
Moshi. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amesema wadudu wanaodaiwa kuwa ni nzige walioonekana katika kijiji cha Karamandei kata ya Toloha wilayani Mwanga walidhibitiwa.
Ameeleza hayo leo Alhamisi Februari 18, 2021 katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Moshi.
"Kulitokea wimbi la nzige Wilaya ya Mwanga uongozi wa Wilaya uliwahi kuijulisha wizara ambayo ilisaidia mapema na bado wanaendelea kuangalia kama kuna dalili zozote za kurudi lakini mpaka leo asubuhi sijaletewa taarifa kama bado nzige wapo au wanaendelea kuleta madhara yoyote."
Kuhusu madhara ya nzige hao amesema walivamie eneo la msitu lenye majani na walibaki eneo hilo.