Royal Tour yatumia fedha za Watanzania

Muktasari:

  •  Rais Samia Suluhu Hassan, leo ametumia tukio la uzinduzi wa filamu ya ‘The Royal Tour’ kuwashukuru Watanzania waliotoa michango yao kuhakikisha utengezaji wa filamu hiyo unafanikiwa.


Arusha. Rais Samia Suluhu Hassan, leo ametumia tukio la uzinduzi wa filamu ya ‘The Royal Tour’ kuwashukuru Watanzania waliotoa michango yao kuhakikisha utengezaji wa filamu hiyo unafanikiwa.

Ameyasema hayo leo Alhamisi Aprili 28, 2022 Jijini Arusha katika uzinduzi wa Royal Tour.

Amesema kuwa kazi yote imefanywa kwa michango ya watanzania, hakuna fedha ya serikali iliyotumika.

“Pesa yote mpaka tumekwenda Marekani na kurudi ni pesa iliyochangwa na watanzania. Kwa hiyo kama tunazungumza the real star (mwigizaji halisi) katika hii filamu ni watanzania wote,”amesema Rais Samia.