Saba wafa kwa kunywa sanitiser Russia

Monday November 23 2020
SANITIZE PIC

Moscow, Russia (AFP)
Watu saba Jamhuri ya Yakutia nchini Russia wamefariki dunia na wengine ni mahututi baada ya kunywa vitakasa mikono vilivyochanganywa, bidhaa ambayyo ilikuwa ikipatikana kwa wingi wakati wa mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya corona.
Taarifa iliyotolewa na wachunguzi nchini Russia Jumamosi ilisema kundi kubwa la watu liliugua ghafla katika kijiji cha Tomtor baada ya kunywa kimiminika hicho kilichochanganywa baada ya kununua katika duka moja la eneo hilo.
Wachunguzi walisema walikuta dumu la lita tano lisilokuwa na chapa katika eneo hilo.
Na uchunguzi wa vipimo baadaye ulionyesha kuwa kimiminika kilichokuwa ndani ya dumu hilo kilikuwa na asilimia 69 ya methanol, aina ya pombe ya kiwandani ambayo haitumiki kama kilevi.
Watu watatu wa kwanza walifariki eneo la tukio,  wakati wengine sita walisafiorishwa kwa ndege kwenda mji mkuu wa eneo hilo wa Yakutsk. Wanne walifariki wakiwa hospitali.
Kwa sasa madaktari wanapambana kuokoa maisha ya watu wawili waliosalia -- mwanamke wa miaka 4 na kijana wa miaka 32, wote wamepoteza fahamu na wanapumulia mashine, mamlaka inayoshughulika na afya ilisema.
Jumapili mamlaka ya afya ya Yakutia ilipiga marufuku uuzwaji wa kitakatisha mikono chenye kemikali ya methanol.
Matumizi ya vimiminika vya bei rahisi vinavyotumika badala ya pombe ni ya kawaida nchini Russia, hasa maeneo wanayoishi masikini.
Mwaka 2016, zaidi ya watu 100 wa eneo la Irkutsk jimbo la Siberia walikunywa sumu iliyokuwa katika losheni ya bafuni, na 78 kati yao walifariki.
Dawa za bafuni pia huwa na methanol ambayo hutengeneza sumu inaovunjwa, na mara nyingi husababishas upofu au kushindwa kupumua.
Ingawa unywaji pombe unapungua nchini Russia, ununuzi uliongezeka kwa kasi mwezi Machi wakati wananchi walipozuiwa kufanya matembezi kutokana na virusi vya corona.
Wakati huohuo, gavana wa Yakutsk amepiga marufuku ya ununuzi wa pombe kwa wiki moja.

Advertisement