Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Safari ya mwisho ya Jenista itakavyokuwa, kuzikwa Desemba 16

Mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Peramiho (CCM), Jenista Mhagama unatarajiwa kuzikwa Jumanne ya Desemba 16, 2025 katika Kijiji cha Ruanda, Mbinga mkoani Ruvuma.

Jenista ambaye amekuwa mbunge wa Peramiho kuanzia mwaka 2005, amefariki dunia jana Alhamisi, Desemba 11, 2025 jijini Dodoma.

Ratiba ya mazishi yake iliyotolewa usiku wa Alhamisi na uongozi wa Bunge, inaonesha kesho Ijumaa, mwili wake utapelekwa nyumbani kwake Itega, jijini Dodoma.

Jumamosi ya Desemba 13, 2025, mwili wa Jenista utapelekwa Kanisa Katoliki Kiwanja cha Ndege itakapofanyika ibada.

Viongozi mbalimbali watahudhuria kanisani hapo wakiwemo Spika wa Bunge, Mussa Zungu, Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba na Makamu wa Rais, Dk Emmanuel Nchimbi.

Baada ya shughuli ya hapo kanisani, mwili wa Jenista utasafirishwa kwenda Songea, Mkoa wa Ruvuma.

Desemba 14, 2025, maombolezo yataendelea nyumbani kwa Jenista, eneo la Makambi, Songea Mjini. Siku hiyohiyo mwili utapelekwa Kanisa Katoliki Matogoro, Songea Mjini ambapo ibada itafanyika na baadaye mwili kurudishwa nyumbani.

Desemba 15, 2025, mwili wa Jenista utapelekwa kwa wapiga kura wale Peramiho ambapo shughuli itafanyika Kanisa Katoliki la Peramiho  ambapo viongozi mbalimbali wanatarajiwa kuwepo akiwemo Zungu, Dk Mwigulu na Dk Nchimbi.

Baadaye mwili utarudishwa nyumbani kwake Peramiho. 

Desemba 16, 2025, mwili wa Jenista utapelekwa Kijiji cha Ruanda ambapo utahifadhiwa katika nyumba yake ya milele.