Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Saratani kwa watoto wa kiume yatikisa KCMC

Saratani kwa watoto wa kiume yatikisa KCMC

Muktasari:

  • Daktari bingwa wa magonjwa ya damu na saratani kwa watoto hospitali ya rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC), Dk Esther Majaliwa amesema asilimia 57   ya watoto wanaokutwa na  saratani ya mfumo wa damu na tezi  ni wa  kiume ikilinganishwa na asilimia 43 ya watoto wa kike wanaobainika kuwa na ugonjwa huo.


Moshi. Daktari bingwa wa magonjwa ya damu na saratani kwa watoto hospitali ya rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC), Dk Esther Majaliwa amesema asilimia 57   ya watoto wanaokutwa na  saratani ya mfumo wa damu na tezi  ni wa  kiume ikilinganishwa na asilimia 43 ya watoto wa kike wanaobainika kuwa na ugonjwa huo.

Amesema wagonjwa wapya 298   ambao ni sawa na asilimia 15.5 waligundulika kwa mara ya kwanza katika hospitali hiyo  kuwa na ugonjwa wa saratani  ambapo asilimia 54 ni watoto  wenye umri chini ya miaka 10.

Ameeleza hayo jana Ijumaa Septemba 10, 2021 katika maadhimisho ya mwezi wa saratani kwa watoto ambayo  kila mwaka hufanyika katika hospitali hiyo.

Katika maadhimisho hayo yaliyokwenda sambamba na matembezi ya zaidi ya kilomita tatu Dk Majaliwa amesema, "tunapata watoto wengi sana wa kiume hapa wenye saratani,    bado hatujajua ni kwa nini lakini kuna utafiti  tunahitaji kufanya kujua sababu  watoto wengi ni  wa kiume."

 “Tukiangalia kutoka mwaka 2016 hadi 2021 hospitali hii ilitibu watoto 2000 wenye saratani na  kati ya hao   298 ni wapya  ambao ni sawa na asilimia 15.5. Asilimia 43.2 ya  saratani tunazozibaini ni za mfumo wa damu na tezi na idadi ya wagonjwa inaongezeka."

"Kikubwa ambacho jamii inapaswa kujikinga na ugonjwa huu hasa kwa watoto wadogo ni chanjo, hizi chanjo ambazo wanapata utotoni zinasaidia kuzuia virusi na magonjwa mbalimbali ambayo yanaweza kumletea mtoto hali ya kupata saratani,” amesema Dk Majaliwa.

Mkurugenzi mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Gileard Masenga ameishukuru Serikali kwa kutenga  Sh4 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa jengo maalum la tiba ya mionzi katika hospitali hiyo na  kwa mwaka  inapokea wagonjwa 5000 hadi 6000.