Selcom Tanzania: Kinara wa hudumu jumuishi za fedha na mageuzi

Kodi mpya za digitali: Mtihani kwa uchumi

Muktasari:

  • Bila shaka yoyote, Tanzania ni moja ya nchi duniani ambazo soko la huduma ya fedha kwa simu za mkononi linakua kwa kasi, lakini suala hilo lilikuwa gumu miaka 15 iliyopita.

Bila shaka yoyote, Tanzania ni moja ya nchi duniani ambazo soko la huduma ya fedha kwa simu za mkononi linakua kwa kasi, lakini suala hilo lilikuwa gumu miaka 15 iliyopita.

Moja ya kampuni ambazo ziliwezesha lisilowezekana kuwezekana ni Selcom Tanzania. Katika mahojiano haya, mwandishi maalum mwandamizi, Costantine Muganyizi anamuhoji Mkurugenzi Mtendaji wa Selcom Tanzania,Sameer Hirji ambaye anaangalia kuhusika kwa kampuni hiyo katika biashara ya fedha kwa njia ya simu za mkononi  iliyokuwa mpya wakati huo hadi ilivyo sasa.

Anaangalia changamoto kama kodi na upangaji bei, huku akiamini kuwa kwa ushirikiano na BoT, Wizara ya Fedha na Mamlaka ya Mawasiliano, uchumi usiotumia fedha taslimu unawezekana Tanzania.

Tuanze mahojiano kwanza kwa kujua nini kilisukuma maono yako ya kidigitali kwa Tanzania and kusababisha ndoto ya kuanzisha kampuni ya Selcom.
JHakukuwa na ndoto hasa, lakini wakati wote kulikuwa na maono na nia ya kufanya kitu katika suala la malipo tangu nikiwa (kampuni ya huduma za simu ya) Celtel.

Mwishoni mwa muda wangu huko, kulikuwa na mazungumzo kuhusu huduma za kifedha kwa njia ya simu za mkononi baada ya M-Pesa kuanzishwa Kenya.

Nafasi ilikuw ainajionyesha Tanzania kutokana na changamoto ya ukosefu wa miundombinu ya kutosha, uunganishwaji wa taarifa, unafuu na USSD (menyu ambayo inatumika katika kujiunga na huduma mbalimbali za simu za mkononi) ya kuaminika na njia za ujumbe mfupi, bila kuacha simu za mkononi zinazofaa zikimilikiwa na watu wengi na haja ya simu za mkononi kujiingiza kw ajamii ili kukuza lengo la kufanya huduma za fedha kwa simu za mkononi kuwa rasmi.  


Kwa mfano, wakati tukishirikiana na Benki ya Posta Tanzania mwaka 2007, ulitakiwa kuandika ujumbe kuangalia salio lako au kutuma fedha kwa mteja mwingine wa TPB.

Ilikuwa njia inayoumiza, ngumu  na yenye usumbufu. Ulitakiwa uwe na kama karatasi ya kukumbuka maneno tofauti ya siri, vifupisho na muundo wa ujumbe.

Hakukuwa na mtozaji, njia za malipo ya kielektroniki ya muda wa maongezi kwa ajili ya kununua; huduma ya kibenki katika simu za mkononi hazikuwa karibu kama ilivyo sasa.


Kwa kuwepo huduma za fedha katika simu za mkononi (MFS), kulikuwa na ushahidi wa matokeo makubwa na wakati kuianzisha huduma hiyo ilichukua muda, kulikuwa na jitihada zilizoimarishwa, zikiungwa mkono na Benki Kuu ya Tanzania, kwa ajili ya kujumuisha Watanzania wengi kadiri iwezekanavyo katika huduma za kifedha, kw aharaka kadiri iwezekanavyo.

Pia kulihusishwa wafadhili wengi, kazi iliyofanywa na FSDT ambayo ilitoa fedha kwa ajili ya kuingiza mawakala wa fedha za simu za mkononi nchi nzima, jambo ambalo liliwezesha kwa kiasi kikubwa kuanzisha huduma hiyo


Kama Selcom, tulikuwa wa kwanza sokoni katika mambo mengi. Kwa kuwa si kila mtu alikuwa na haja kubwa ya kutuma fedha kwa nduguye kijijini, tulipata njia za kufanya zaidi katika huduma ya fedha katika simu za mkononi kuliko kuwa na P2P pekee.

Selcom ilikuwa ya kwanza kuuza LUKU kwa kutumia simu za mkononi, si tu nchini Tanzania bali barani Afrika. Pia tulikuwa wa kwanza kuwezesha uhamishaji fedha kutoka benki hadi kwenye simu (bank2wallet) na kutoka kwenye simu hadi benki

Selcom Tanzania: Kinara wa hudumu jumuishi za fedha na mageuzi

(wallet2bank), na hali kadhalika wa kwanza kuwezesha fedha katika simu za mkononi kuweza kuhamishwa kutoka kampuni moja hadi nyingine katika mradi elekezi kati ya huduma ya Airtel Money na Tigo Pesa, kazi yetu kubwa ikiwa ni njia ya kuongozea ikolojia nzima kutokana na kutokuwepo na mfumo wa kitaifa.  
 
Ni kwa kiasi gani wazo hili jipya limefanikiwa na nini kitegemewe kutoka kampuni yenu huko mbeleni?   


Kusema kweli tumekuwa wataalamu katika kuongoza na kukua kama biashara, kutoka kuwa dalali (neno ambalo binafsi linanikera) au ofisi saidizi ya utoaji huduma, kuwa kampuni ambayo sasa inazungumza na wateja moja kwa moja.

Teknolojia na njia zetu zimekuwa zikitumiwa kuwezedsha wateja wetu, ambayo baadaye tuliona ilikuwa ikitukwamisha, au ikituharibia kwa sababu wateja wetu baada ya muda wakaanza kufikiria kutuondoa katika mnyororo wa thamani kwa kuchukua jukumu letu na kulifanya wao wenyewe ili kupunguza gharama au kukuza mapato.

Nadhani hiki ni kitu kizuri kukifikiria kwa upande wao, lakini matokeo ikatusukuma kutafuta na kutumia njia nyingine kwa ajili ya kurejesha biashara na mapato yaliyopotea, mara nyingi kama washindani wa wateja tunaowahudumia.

Hiki si kitu tulichokusudia lakini ndio mwelekeo wa ujumla ambako huduma za kifedha zinaelekea - kwanza kwa kuachana na watoaji huduma waliokuwepo na baadaye kujenga huduma inayovutia zaidi, inayofikiwa zaidi na nafuu, ambayo inaweza kuwa nzuri kwa ushindani na bora kwa mtumiaji.  
 
Kwa nini Selcom inasifiwa kwa kubeba jukumu la kuongoza safari ya mabadiliko ya kidigitali Tanzania na kukuza ujumuishaji wa kifedha nchini?


Sawa kabisa, kusema kweli, kwa sababu tulifanya hivyo, lakini nadhani hatupati sifa za kutosha kwa kazi tuliyofanya na tunaendelea kuifanya katika suala hili.

Mabadiliko ya kidigitali kama haya yalianza wakati tulipoanzisha soko saidizi la malipo ya fedha taslimu. Selcom inagusa kugeuza malipo ya fedha taslimu kuwa ya kidigitali, hadi kufikia malipo ya kutumia simu za mkononi na malipo kwa kadi.

Tumeona mabadiliko kutoka kupanga mstari katika matawi ya benki na kulipia muda wa maongezi na umeme, hadi kufikia kuwezesha mawakala ambao waliweza kufanya malipo hayo kwa niaba ya wateja, kuokoa muda na juhudi.

Kazi yetu imetuwezesha tufanye kazi na kila mdau katika mnyororo wa thamani wa huduma za kifedha, hali kadhalika sekta binafsi. Changamoto ya mteja leo inaweza kuwa rahisi au ngumu kama ilivyo kuingia katika ERP, programu inayosimamia na kuunganisha taarifa za fedha, au mifumo ya usimamizi wa fedha - na tunashughulikia eneo lote la mahitaji hayo kwa kutumia API ambayo ni rahisi kutumika.

API ni programu tumishi ambayo inatambua programu tumishi nyingi.  
Mawakala wetu wanaweza kufikia sehemu zilizo vijijini sana kuhudumia wateja wa benki wanaoweka na kutoa fedha, wakati alama zetu za utambuzi kwa ajili ya huduma ya Selcom Pay, zinaweza kupatikana maduka yote ya bidhaa bora nchini Tanzania - kwa makisio yangu soko bado halijafikiwa kikamilifu, na bado tunahitaji kuwafikia wateja ambao hawajazoea huduma hizi kama mama ntilie, au hata waendesha bodaboda. Lengo letu ni kwamba ukubwa wowote wa biashara au mjasiriamali mmoja ajue ni jinsi gani ya kutumia, kukusanya na kuhifadhi kidigitali, bila ya hata kutegemea fedha taslimu au akaunti ya benki ambayo ina gharama.
 
Kwa zaidi ya miaka kumi, sekta ya malipo ya kidigitali nchini imejikita kusaidia vitu kama malipo ya kibiashara na hivyo kuwa na ukuaji mkubwa unaoifanya Tanzania kuwa na moja ya masoko yanayokua kwa kasi duniani.

Kwa mukhtadha huo wa huduma na uendeshaji wa Selcom, kwa kifupi inaonekana kiwango ambacho malipo yasiyotumia fedha taslimu nchini na nani anatakiwa afanye nini kuyapeleka katika kiwango cha juu Zaidi?
Kikwazo kikubwa kwa sasa ni gharama za miamala kwa kampuni ndogo na za kati na mashirika.

Kuna chembechembe zinazoonyesha kuzidisha utozaji fedha kwa sababu tofauti na hivyo kuingiza migongano isiyo muhimu katika ikolojia. Wakati kuna kiwango fulani cha mifumo kubadilisha taarifa na kuzitumia (interoperability), hakuna kitu ambacho ningekiita “seamless interoperability”.

Bado tuna walinzi na uzio ambao unahitaji kuondolewa ili malipo yawe yamefungamana kikamilifu na ushiriki  usiwe na mashaka. Kuongeza kasi ya ushiriki hadi kufikia kiwango cha juu kunahitaji kushughulikia masuala ya kisheria, na naisifu Benki Kuu ya Tanzania kwa kushughulikia TIPS (mfumo wa malipo ya haraka) ili sekta iweze kukabiliana na sheria na hivyo kutatua tatizo la bei zinazoumiza, makubaliano baina ya pande mbili na kupata kwa tozo bila ya sababu za msingi.

Kwa upande mwingine, bado chini ya Wizara ya Fedha, utozaji kodi katika miamala unahitaji kutathminiwa kuanzia chini ili ushiriki katika uchumi wa kidigitali usionekane mzigo wa gharama kwa mtumiaji  au kikwazo kwa ushiriki endelevu katika eneo hili.

Kuna hisia zisizovumilika za kupukutika kwa fedha za watumiaji wakati wanapotozwa kodi kupita kiasi wanapotumia huduma za kidigitali.

Nini maoni yako kuhusu malengo ya Tanzania katika uchumi usiotumia fedha taslimu na maendeleo yake kuelekea matumizi ya fedha za kidigitali kikamilifu?  


Hili ni suala la kidunia, na tunaondesha wimbi hili Tanzania. Tuna huduma ya fedha za simu za mkononi na hii ni pale sehemu kubwa ya miamala inayofanyika leo imekuwa msaada mkubwa wa kufikia na kukuza ujumuishaji wa kifedha, lakini hatuna budi kufikiria mbali zaidi. Tunahitaji kufikiria kuhusu inamaanisha nini kuwa na uchumi wa kidigitali usiotumia fedha taslimu.

Hatuna budi kugusa katika kila ngazi ya uchumi, kwa sababu wakati kuna ujumuishaji wa kifedha, kunaweza kusiwe na ujumuishaji wa kidigitali. Tunahitaji ujumuishaji wa kidigitali ili kwamba hata wakati nanunua mboga za majani, natakiwa niwe nimehakikishiwa muuzaji atakubali malipo ya kielektroniki, na hili linaweza kufikiwa tu kama wadau wote katika mnyororo wa thamani watakubaliana na maono hayo.

Malipo kutoka kwa mtumiaji kwenda kwa mfanyabiashara, kwenda kwa mgavi, kwenda kwa mkulima, kwenda kwa mtoaji wa pembejeo na kwenda kwa muagizaji hayatakiwi kuhusisha fedha taslimu kabisa - hicho ndicho kikombe kitakatifu tunachokitaka.  
 
Je hali ya sera za sasa inasaidia vya kutosha kuwapa wadau wa fedha za kjidigitali fursa ya kuihudumia nchi na kusaidia kujumuisha wasiotumia  huduma hizo waingie katika mfumo rasmi wa kifedha?


Tunafanya kazi na waratibu wawili wazuri. Benki Kuu ya Tanzania ni taasisi ya vitendo, inafikiria mbele na pengine ndiyo msimamizi anayekuwa wa kwanza nchini katika kuchukua na kuwezesha mawazo mapya, ubunifu, uendelezaji wa ujumuishaji wa kifedha na kwenda na wakati katika muda huu ambao mambo na mazingira yanabadilika kwa kasi.

Benki Kuu inaimarisha sheria wakati wote, ikiazima na kuiga mifano bora duniani kwa ajili ya kuboresha mkakati wetu wa taifa wa ujumuishaji kifedha.


Mamlaka nyingine tunayofanya nayo kazi ni (Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania) TCRA. Hii imekuwa msaada mkubwa katika mipango yetu ya ukuaji tangu siku za mwanzoni.

Mamlaka hii ina uzoefu wa kutosha na changamoto zinazoikabili sekta yetu wakati huu tunaposukuma suala la ukuaji wa miundombinu, suala la kujua maeneo yaliyo na huduma na huduma bora zaidi za kiposta na usafirishaji vifurushi, mtandao wa kasi na upatikanaji wa mhimili wa taarifa.

Ni kwa jinsi gani Watanzania wa kawaida wamenufaika na uwekezaji ambao Selcom imekuwa ikiufanya kusukuma ajenda ya taifa ya ujumuishaji kifedha?


Nadhani kama Selcom, tunaweza kufanya mengi zaidi ya tunayofanya leo. Ingawa tumefanya kazi kubwa na kuwekeza katika mifumo na miundombinu, wakati wote tumekuwa wawezeshaji kwa wateja wetu. Kufikia uwezo wetu kikamilifu kunahitaji kwenda moja kwa moja kwa mteja, na hicho ndicho tutakijenga huko mbele. Tunaona thamani kubwa kwa kulifanya hili na soko ambalo halijafikiwa. Kuna utengenezaji mkubwa wa thamani wakati unapounda mkakati wako binafsi.

Kwa sasa, tunaweza kukua tu kwa kasi kutegemeana na wateja wetu wanavyoturuhusu. Kwa hiyo hatujafikia kikamilifu malengo yetu.
 
Na ategemee nini kutoka kampuni yenu baadaye kwa kuangalia kukuza ufanisi na kupunguza gharama zinazohusisna na miamala ya kifedha ambayo ndiyo hasa hali ya jamii isiyotumia fedha taslimu?


Tayari Selcom ni taasisi inayojifunza ikiwa na muundo ulio tambarare ambao unafanya gharama zetu kuwa chini.

Tunaendeleza ukuaji na kuangalia biashara yetu kwa kutumia darubini kubwa, hivyo matokeo ya hilo, kila punguzo tunalofanya kwa sababu ufanisi wetu, linagusa moja kwa moja wateja wetu. Hii ni moja ya sababu ya huduma zetu kuwa nafuu, na tumekuwa tukiangalia jinsi tunavyopanga bei za huduma zetu.

Fikra za sekta kwa ujumla kuhusu upangaji bei zinabidi kubadilika, hasa kwa jinsi tunavyotengeneza fedha kwa kutumia huduma zetu. Kuna njia nzuri zaidi na za kiakili zaidi za kutengeneza fedha bila ya kuhamishia mzigo bila ya sababu kwa mteja.

Nani wamekuwa washirika wa Selcom katika safari yake ya mabadiliko ya kidigitali na ni manufaa gani ushirikiano huu umefanikiwa kuleta kwa mtu mmojammoja, kampuni au katika ngazi ya sekta?


Washirika wakubwa kuliko wote wamekuwa ni wasimamizi. Mpangilio wetu wa kiteknolojia ni suala la umiliki na hivyo tuna wachache, utegemezi wa nje wa upande au wauzaji.

Kwa hiyo, naisifu sana timu ya Selcom kwa kufanya kazi bila ya kuchoka na kila siku kufikia ndoto yetu na kwa kutusaidia kufika hapa tulipo leo.
 
Mwisho, kwa kifupi unaweza kutaja mipango yenu ya kidigitali na shughuli zenu nje ya Tanzania?


Tuna ushirikiano wa kimkakati na Mastercard ambao umetuwezesha kuingia katika masoko kadhaa.

Tayari tunafanya nao kazi ya kujenga jukwaa na miundombinu ili kuweka njia muhimu za kukuza malipo ya wafanyabiashara, utoaji wa kadi, kuchukua na huduma nyingine za ziada pamoja na mali nyingine kutoka Mastercard.

Hii inatupa mteja-kinara wa kufanya naye kazi katika masoko hayo na matokeo yake inaturuhusu kutia mguu katika mlango kutoka pale tunapoweza kujenga nyayo zetu wenyewe barani (Afrika). Kuna masoko 11 mezani na tunatazamia kuwa katika kila soko ifikapo mwishoni mwa mwaka kesho.