Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali ikipata Sh45.5 bilioni gawio NMB

Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya NMB, Ruth Zaipuna

Dar es Salaam. Kiasi cha Sh143.1 bilioni kimetolewa kama gawio na benki ya NMB katika mwaka wa fedha 2022 ikiwa ni ongezeko la asilimia 48 ikilinganishwa na Sh96.7 bilioni zilizotolewa mwaka 2021.

Gawio hilo ambalo limetolewa kwa makundi matatu ya wanahisa ikiwemo Serikali ambayo inamiliki asilimia 31.8 ya hisa imepata Sh45.5 bilioni.

Mwanahisa mwenza katika benki hiyo kampuni ya Arise BV inayomiliki asilimia 34.9 imepata Sh49.9 na wanahisa wengine kwa ujumla yao wanamiliki asilimia 33.3 wamepata Sh47.7.

Akizungumza leo wakati wa hafla ya utoaji gawio kwa Serikali Ofisa Mtendaji Mkuu wa NMB Ruth Zaipuna amesema gawio kwa serikali limeendelea kuongezeka kutoka Sh4.9 bilioni mwaka 2009 hadi kufikia Sh45.5 bilioni kwa mwaka wa fedha 2022.

Ongezeko hili ni sawa na asilimia 911 na inafanya gawio hili kuwa kubwa zaidi kutolewa na taasisi yoyote ya kifedha kwa Serikali kupitia uwekezaji wake kupitia kwa msajili wa hazina.

“Tayari fedha hizi zimeshawekwa kwenye akaunti ya ofisi ya msajili wa hazina, pia mwanahisa mwenza na wanahisa wengine kwa ujumla wao wameshalipwa,”

Amesema pamoja na gawio NMB imerejesha kodi Serikalini katika kipindi cha mwaka 2022 kiasi cha Sh453 bilioni.

“Nidhamu yetu wa urejeshaji kodi kwa Serikali na mchango thabiti katika maendeleo ya uchumi na kijamii kupitia ulipaji wa kodi umeifanya kuwa mlipa kodi mkubwa zaidi,” amesema Ruth.

Katika kuadhimisha miaka 25 ya benki ya NMB, Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Ruth Zaipuna ametangaza kuwa wametenga kiasi cha Sh2.5 bilioni kwa ajili ya kujenga shule ya mfano katika mkoa utakaolekezwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Hatua hiyo inalenga kuunga sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali za kuinua sekta ya elimu nchini.