Serikali kugharamia mazishi waliofariki ajalini Tanga
Muktasari:
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omary Mgumba amesema Serikali itagharamia mazishi ya familia ya watu 17 waliofariki kwa ajali ya gari wilayani Korogwe mkoani Tanga.
Tanga. Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omary Mgumba amesema Serikali itagharamia mazishi ya familia ya watu 17 waliofariki kwa ajali ya gari wilayani Korogwe mkoani Tanga.
Ajali hiyo ilitokea jana usiku katika eneo la Magira Gereza, wilayani hapo barabara ya Segera-Buiko na kusababisha vifo hivyo pamoja na majeruhi 12.
Ndugu hao walikuwa wakisindikiza mwili wa mwanafamilia mwenzao, Athanas Mrema (59) aliyefariki dunia Februari Mosi, kutoka Dar es Salaam kuelekea mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza leo Jumamosi Februari 4, 2023 katika Hospitali ya Magunga wilayani hapo amesema Serikali itagharamia mazishi ya familia hiyo.