Serikali kusamehe kodi kwenye simu janja, vishikwambi na modemu

Thursday June 10 2021
mujanjapic

“Sekta ya mawasiliano imekuwa ikikua vizuri na kuwa kiungo muhimu cha kuongeza wigo wa wananchi ambao wako kwenye ulimwengu wa kidijitali na kwenye sekta ya fedha. Napendekeza kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye simu janja za mkononi HS Code 8517.12.00, vishikwambi (Tablets) HS Code 8471.30.00 au 8517.12.00 na modemu (modems) HS Code 8517.62.00 au 8517.69.00. Lengo la hatua hii ni kuhamasisha matumizi ya huduma za mawasiliano ili kufikia lengo la asilimia 80 ya watumiaji wa intaneti ifikapo mwaka 2025 kutoka asilimia 46 iliyopo sasa,” amesema Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba.

Advertisement