Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali ya Tanzania yaweka msimamo kuhusu mashamba

Muktasari:

Waziri wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda amesema kuanzia sasa mashamba yote ambayo serikali ina dhamana nayo moja  moja hayatalimwa mazao mengine zaidi ya ngano na shayiri.


Siha.Waziri wa Kilimo nchini Tanzania, Profesa Adolf Mkenda amesema kuanzia sasa mashamba yote ambayo Serikali ina dhamana nayo hayatalimwa mazao mengine zaidi ya ngano na shayiri.

Mkenda ameyasema hayo alipotembelea mashanba ya wakulima wa West Kilimanjaro yaliyopo wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro.

"Mashamba ambayo serikali ina dhamana nayo moja kwa moja hatutaruhusu tena mazao mengine,   tunakwenda kwenye kwenye kilimo cha ngano na shayiri ilimradi unapolima tutahakikisha kuna soko zuri ambalo litakusaidia,"amesema Profesa Mkenda.

Profesa Mkenda amesema Serikali inachofanya ni kuongeza jitihada za kupata mbegu bora na kuongeza uzalishaji kwa kasi wa upatikanaji wa mbegu bora ili ziweze kusambazwa kwa wakulima.

"Serikali tutakacho kifanya ni kuhakikisha mnapata bei nzuri na kupata uhakika wa masoko kwa ajili ya kuuza mazao haya, tutaongeza uzalishaji wa mbegu hizi ili tusambaze kwa wakulima wote nchini," amesema Profesa Mkenda

"Habari njema ni kwamba sasa hivi ukilima ngano na shayiri soko la uhakika lipo, tumeshakubaliana na waagizaji wa ndani ambao wanatengeneza ngano kwamba kabla hawajaagiza nje wanunue kwanza ngano yote iliyopo nchini."