Serikali yafuta mashirika yasiyo ya kiserikali 4,879

Muktasari:

  • Serikali imeyafuta mashirika yasiyo ya kiserikali 4,898  kati ya hayo yapo yaliyoomba kuacha shughuli zao kwa hiari

Dar es Salaam. Serikali imeyafuta mashirika yasiyo ya kiserikali 4,898  kati ya hayo yapo yaliyoomba kuacha shughuli zao kwa hiari.

Taarifa ya kufutwa kwa mashirika hayo  imetolewa Januari 24, 2022 na Kaimu Kitengo cha Mawasiliano Serikali, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Atley Kuni katika taarifa yake amesema kati ya mashirika hayo,  4,879 yamefutwa kutokana  na ukiukwaji wa sheria, kanuni na miongozo inayosimamia shughuli za mashirika hayo.

Mashirika 19 yamefutwa usajili wake baada ya kuomba kusitisha shughuli zao kwa hiyari.

“Maamuzi hayo yemefikiwa na bodi ya mashirika yasiyo ya kiserikali katika kikao chake cha 49 kulichofanyika Januari19, 2023 jijini Dodoma,”ilisema sehemu ya taarifa hiyo na kuongeza kuwa hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 7(1) cha sheria ya mshirika yasiyo ya kiserikali sura ya 56 ya sheria za Tanzania.

Hata hivyo, bodi hiyo inayoongozwa na mwenyekiti wake Mwantumu Mahiza, imeatoa wito kwa mashirika yasiyo ya kiserikali kufanya kazi zao kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo mbalimbali ya uratibu wa mashirika ya kiserikali ili yaweze kufikia malengo yaliyokusudiwa ya kuwahudumia wananchi wa Tanzania.