Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali yakanusha hospitali kujaa wagonjwa wenye shida ya mfumo wa hewa

Serikali yakanusha hospitali kujaa wagonjwa wenye shida ya mfumo wa hewa

Muktasari:

  • Katibu Mkuu Wizara ya Afya nchini Tanzania, Profesa Mabula Mchembe amesema hospitali hazijajaa wagonjwa wenye shida ya mfumo wa hewa kama inavyoelezwa, akibainisha wengi wapo katika wodi za upasuaji.

Moshi. Katibu Mkuu Wizara ya Afya nchini Tanzania, Profesa Mabula Mchembe amesema hospitali hazijajaa wagonjwa wenye shida ya mfumo wa hewa kama inavyoelezwa, akibainisha wengi wapo katika wodi za upasuaji.

Profesa Mchembe ameyasema hayo leo Jumamosi  Februari 13, 2021 alipofanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC) pamoja na kuangalia mwenendo wa utoaji wa huduma za afya katika hospitali hiyo.

"Wafanyakazi wanaohudumia wagonjwa wenye matatizo ya mfumo wa hewa wana afya njema wala hawajapata matatizo. Ukiangalia hospitali sio kama wanavyosema kwamba zimejaa wagonjwa wenye matatizo ya mfumo wa hewa, hapa nimekuta wagonjwa wengi zaidi katika wodi za upasuaji," amesema Profesa Mchembe.

Amebainisha kuwa kwa sasa wataongeza nguvu katika upande wa upasuaji ili wananchi wasikae hospitali kwa muda mrefu.