Sh23.9 bilioni kufanya matengenezo ya barabara Morogoro

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka leo Jumatatu Aprili 17, 2023 akizungumza na waandishi wa habari juu ya utekelezaji wa mradi wa barabara ya Rudewa hadi Kilosa.

Muktasari:

  • Wakati matengenezo ya barabara katika mkoa wa Morogoro yakilamba Sh23.9 bilioni Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) imewataka wananchi kulinda miundombinu ya barabara ikiwemo alama zinazowekwa ili kuepusha ajali zinazoweza kutokea.

Morogoro. Wakati Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Mkoa wa Morogoro ikitengewa Sh23.9 bilioni katika mwaka wa fedha 2022/2023 kwa ajili ya matengenezo ya barabara ya kawaida na kinga za uharibifu katika madaraja, wananchi wametakiwa kutunza alama za barabarani ili kuepusha ajali zinazoweza kutokea.

Hiyo ni kutokana na kile kilichoelezwa kuwa baadhi ya wananchi wamekuwa na tabia kung'oa alama za barabarani jambo ambalo linaweka maisha ya madereva hatarini.

Hayo yaneelezwa na Kaimu Meneja wa Tanroads Mkoa wa Morogoro, Mussa Kaswahili wakati akielezea utekelezaji wa utengenezaji wa miundombinu uliofanyika ndani ya mkoa huo ikiwemo ujenzi wa Barabara ya Rudewa hadi Kilosa.

Kaswahili alisema Serikali imekuwa ikiendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuhudumia barabara ndani ya mkoa huo ili kuhakikisha zinapitika nyakati zote za mwaka.

"Pia jiografia ya Mkoa wa Morogoro ni ya milima na makorongo mengi ina madaraja 1,032 na mtandao wa barabara ni km 2,070. Barabara ya Morogoro - Dodoma pekee hutumia takribani asilimia 17 ya bajeti ya matengenezo," amesema.

 Akizungumzia ujenzi wa daraja la Kiyegeya uliofanyika amesema umetumia teknolojia sawa na ile ya daraja la Ubungo jijini Dar es Salaam kutokana na umuhimu wake katika usafirishaji wa watu na bidhaa.

Ujenzi wa daraja la Kiyegeya ulifanyika mwaka 2020 baada ya ya kingo zake kusombwa maji katika eneo la Gairo barabara ya Morogoro-Dodoma.

Kutokana na umuhimu wake katika kuunganisha mikoa na nchi za jirani Serikali Iliingia katika mpango wa dharula kwa kutenga Sh6.9 bilioni ili kutekeleza ujenzi wa daraja jipya ulioanza rasmi Novemba 5, 2020.

"Daraja hili lina urefu Mita 25 na upana wa mita 12 na kina cha mita 15 pia kujumuisha maingilio ya barabara (approach road) zenye urefu kwa kilomita 1 ambapo mita 600 upande wa kuelekea Dodoma na mita 400 upande wa kuelekea Morogoro," amesema.

Wakati kila kitu kikiwa tayari kwa matumizi, Kaswahili alitumia nafasi hiyo kuwataka wananchi wa mkoa wa Mororogoro kulinda miundombinu iliyotengenezaa ili iweze kisaidia usafirishaji na shughuli za kiuchumi

"Kuna samani nyingi za barabarani zinazoonyesha matuta, milima, ukomo wa speed, madaraja, kona, alama hizi zote ni mawasiliano kati ya mwenye chombo cha moto na wananchi wanaotumia barabara," amesema.

"Hizi tukilinda tunaweza kuimarisha na kupunguza ajali ambazo si za lazima na mikoa wetu na kuokow maisha ya watu wanaopotea kila mara katika vyombo vya moto katika barabara hizi," alisema Kaswahili.

Kuhusu barabara ya Rudewa hadi Kilosa, iliyo na urefu wa Kilomita 24 imetumia Sh32.9 bilioni na mpaka sasa umefikia asilimia 90 baada ya kuanza kujengwa mwaka 2019 na kutarajiwa kukamilika Julai 2023

Akizungumzia umuhimu wake, Shaka Hamdu Shaka ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kilosa amesema Serikali inaendelea kufanya jitihada katika uboreshaji wa miundombinu ikiwemo ujenzi wa barabara ya Rudewa hadi Kilosa.

"Ujenzi wa barabara hii unaenda sambamba na ujenzi wa reli ya kisasa inayokaribia kuisha, eneo la Kilosa ni wanufaika wakubwa wa utekelezaji mkubwa wa mradi huu, wakati ukikamilka yalo maandalizi ya msingi yanayotakiwa kufanywa ili mradi ukiwnza uende sambamba na kuwarahisishia wananchi kupata huduma bora," amesema.

Alisema hilo lilifanya miundombinu ya barabara ya zamani kufanyiwa ukarabati na maeneo korofi yanafanyiwa ujenzi na kukamilka.

"Ni barabara iliyojengwa katika viwango na wakandarasi wazalendo tunaamini kuwa kipande kilichobakia kitafanyiwa kazi.